ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 10, 2018

SUGU URAIANI TENA.


CHANZO/MWANANCHI
Mbeya. Saa chache baada ya kutoka jela, mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu amesema ni mfungwa wa kisiasa, “nilifungwa kiholela na nimetoka kiholela.”
Viongozi wa Chadema wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe leo Mei 10, 2018 walifika katika Gereza Kuu la Ruanda mkoani Mbeya kuwapokea Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga lakini walipigwa chenga ya mwili baada ya kuelezwa na askari magereza kwamba wameshatoka, hivyo kulazimika kuwafuata nyumbani. 
Akizungumza na MCL Digital leo Sugu amesema, “Sikutaka kuhoji sababu za kutolewa, jana niliambiwa jiandae kesho (leo) tutatoka, basi nasi tukasema haina shida kwa sababu sikuwa na sababu ya kuwa ndani. Naamini sikutakiwa kuwa gerezani.”
Sugu akiwa na Masonga alifika nyumbani kwake na kumkuta mlinzi pekee kutokana na mkewe Happiness Msonge kwenda Gereza la Ruanda kuwapokea.
Dakika chache baadaye Happiness na mke wa Masonga, Grace Malya walifika nyumbani hapo na kuwalaki kwa furaha huku wakikumbatiana na kucheka.
Akizungumzia mazingira ya kuachiwa kwa wawili hao, Mbowe amesema, “inaonyesha hawakuwa na sababu ya kuwepo gerezani maana mazingira ya kutolewa kwao ni tata sana.”

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.