ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, May 9, 2018

RC MAKONDA ATOA ANGALIZO KWA WAKANDARASI "WAPIGAJI"

 Na Zephania Mandia wa g.sengo tv.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewaonya wakandarasi wenye tabia ya kutengeneza Barabara za chini ya kiwango na kuharibika ndani ya muda mfupi jambo linalosababisha hasara kwa serikali na usumbufu kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri. 

RC Makonda ametoa onyo hilo wakati wa hafla ya utiaji wa saini kwa Mikataba Nane ya mradi wa matengenezo ya Barabara, Mifereji ya Maji na Culvets inayotekelezwa na Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini TARURA yenye tahamani ya zaidi ya Billion 5.8 ambapo amewataka TARURA kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ujenzi wa barabara hizo.

Aidha RC Makonda amezitaja Barabara zitakazojengwa kupitika mradi huo kuwa ni pamoja na Tegeta Nyuki, Msasani, Magomeni Makuti,Migombani, Kimara baruti, Kibanda cha Mkaa, Sheikh Bofu, Kwa Komba, Msigani, Sea clif na Mwananyamala Kisiwani.

Hata hivyo RC Makonda ametoa wiki mbili kwa TARURA kuhakikisha wakandarasi waliojenga barabara chini ya kiwango zinajengwa upya kwa gharama ya mkandarasi ikiwemo barabara ya Mabatini ambapo barabara hizo zitakuwa na mifereji ya maji, sehemu za watembea kwa miguu na Taa za Barabarani. 

Pamoja na hayo RC Makonda amesema katika uongozi wake hawezi kufumbia macho matumizi mabovu ya fedha za walipa kodi hivyo atahakikisha anasimama kidete kuhakikisha Dar es salaam inakuwa na barabara zenye ubora.

Sanajari na hayo RC Makonda ametaka uwepo wa ushirikiano wa kikazi baina ya TARURA, TANROAD, TANESCO, DAWASCO na TTCL ilikupunguza ucheleweshaji wa miradi na ujenzi usiofuata taratibu unaopelekea uharibifu wa miundombinu. 

LENGO LA RC MAKONDA NI KUHAKIKISHA PESA YA WALIPA KODI INATUMIKA KUONDOA KERO WANANCHI

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.