ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, May 28, 2018

MBAO 1-1 RUVU MCHEZO WA MWISHO LIGI KUU VODACOM TZ BARA



GSENGOtV
Mbao FC imetoka sare ya 1-1 na Ruvu Shooting Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza. (Cheki video kwa muhtasari ikiwemo goli la kusawazisha la Mbao Fc)

MATOKEO MENGINE.
SIMBA SC imefanikiwa kumaliza msimu kwa kupoteza mechi moja tu, baada ya sare ya 1-1 na wenyeji Maji Maji FC Uwanja wa Maji Maji mjini Songea. 

Hiyo inakuwa sare ya tisa ya msimu, mechi nyingine Simba SC ikishinda 20 na kufungwa moja tu na Kagera Sugar mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli wiki iliyopita Uwanja wa Taifa. 


Maji Maji FC leo walitangulia kwa bao la mshambuliaji Marcel Boniventusa Kaheza kabla ya kiungo kutoka Rwanda, Haruna Niyonzima kusawazisha kwa penalti.


Niyonzima aliyesajiliwa msimu huu kutoka kwa mahasimu wa jadi, Yanga alipoteza nafasi ya kuifungia bao la ushindi Simba baada ya mkwaju wake wa penalti kupanguliwa na kipa Hashim Mussa kipindi cha pili.


Ndanda FC imeshinda 3-1 dhidi ya Stand United Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara na kunusurika kushuka daraja.

Kagera Sugar imepata ushindi wa 2-1 mbele ya wenyeji, Lipuli FC ya Iringa Uwanja wa Samora, Tanzania Prisons imeilaza 1-0 Singida United Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, Mtibwa Sugar imetoka sare ya 0-0 na Mbeya City Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro, Mwadui FC imewapiga wenyeji, Njombe Mji FC 2-0 Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe.


Kwa matokeo hayo, Simba SC inamaliza msimu na pointi 69 baada ya mechi zake 30, wakati Azam FC yenye pointi 55 za mechi 29 wapo nafasi ya pili mbele ya mabingwa wa msimu uliopita, Yanga SC wenye pointi 52 za mechi 29.

Mechi kati ya Yanga na Azam FC iliyopigwa majira kuanzia Saa 2:00 usiku wa leo Uwanja wa Taifa na ndiyo imekuwa ya mwisho kuamua mshindi wa pili wa msimu huu. Azam wanataka walipaswa kupata sare tu kuinyakuwa nafasi hiyo. Lakini badala yake wameitandika Yanga kwa jumla ya magoli 3-1.   


Maji Maji na Njombe Mji FC ziimeshuka Daraja kutokana na tayari African Lyon, KMC, JKT Tanzania za Dar es Salaam, Coastal Union ya Tanga, Alliance Schools ya Mwanza na Biashara United ya Mara zimekwishapanda kuelekea ligi ya msimu ujao, itakayokuwa na timu 20 ambayo ni ongezeko la timu nne.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.