ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, May 7, 2018

MAPOROMOKO YA UDONGO YAUWA 18 RWANDA, MVUA KAZI ZAENDELEA KUNYESHA.

Maporomoko ya udongo yauwa watu 18 Rwanda, mvua kali zinaendelea kunyesha



CHANZO/PARStODAY
Maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa yameuwa watu 18 katika mikoa ya kaskazini na magharibi mwa Rwanda mwishoni mwa wiki na kuifanya idadi ya watu walioaga dunia tangu mwezi Januari mwaka huu kutokana na mvua kali nchini humo kuwa zaidi ya 200.
Philippe Habinshuti, Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma na Hatua za Dharura katika Wizara ya Kushughulikia Maafa na Wakimbizi ya Rwanda amesema leo kuwa mvua kubwa zilizonyesha usiku wa jana kuamkia leo zimeuwa watu 15 katika mikoa ya magharibi na kaskazini mwa nchi hiyo.

Phililippe Habinshuti, Afisa wa Kitengo cha Maafa na Huduma za Dharura wa Rwanda.


Habinshuti ameongeza kuwa miezi minne ya karibuni imekuwa mibaya zaidi kuliko kipindi cha mwaka jana na miaka mingine iliyopita.  Aidha watu watatu waliaga dunia mapema jana wilayani Rubavu nchini Rwanda.
Leo Jumatatu watu wamekuwa wakijaribu kuchimbua udongo wa matope kuwatafuta watu waliotoweka huko magharibi mwa Rwanda ambapo watu watatu hawajulikani waliko hadi sasa na sita wamejeruhiwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.