ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 4, 2018

WATU WENYE SILAHA WAVAMIA OFISI ZA SHIRIKA LA MSALABA MWEKUNDU MJINI MOGADISHU SOMALIA.

Watu wenye silaha wavamia ofisi za shirika la Msalaba Mwekundu mjini Mogadishu Somalia



Watu wenye silaha jana walizivamia ofisi za Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu za Mogadishu, mji mkuu wa Somalia na kumteka nyara muuguzi mmoja wa kike, raia wa Ujerumaini.
CHANZO/PARStODAY
Jeshi la polisi linaendelea na operesheni ya kumtafuta Bi Sonja Nientiet aliyetekwa nyara na watu wennye silaha katika ofisi wa shirika la Msalaba Mwekundu mjini Mogadishu.
Tukio hilo lilitokea Jumatano jioni baada ya watu wenye silaha kuvamia eneo hilo na kumteka nyara muuguzi huyo na kutoroka naye mlango wa nyuma ili kukwepa kuonekana na walinzi wa ofisi hizo. 

Ofisi za shirika la Msalaba Mwekundu mjini Mogadishu Somalia
Muuguzi huyo amekuwa akilifanyia kazi Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu tangu mwaka 2014 katika maeneo yenye vita ikiwemo Syria na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. 
Utekaji nyara huo ni tukio la pili kubwa lililowahusisha wafanyakazi wa afya nchini Somalia wiki hii baada ya mfanyakazi mwingine wa Shirika la Afya Duniani WHO, Mariam Abdullahi kutekwa nyara siku ya Jumanne.
Msaidizi wa shirika la Msalaba Mwekundu, nchini Somalia, Daniel O’Malley, amesema: "Tuna wasiwasi mkubwa na usalama wa mwenzetu huyo."
"Ni muuguzi ambaye amejitolewa kuokoa maisha ya watu kila siku na kuboresha kiwango cha afya katika baadhi ya maeneo yenye matatizo mengi zaidi nchini Somalia."
Hadi hivi sasa hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika na uvamizi huo, ingawa matukio kama hayo mara nyingi hufanywa na genge la kigaidi la ukufurishaji la al Shabaab.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.