ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 3, 2018

ALI KIBA, DIAMOND NA BEN PAUL WATAJWA WAKATI BABU SEYA NA MWANAE WAKIIBUSU ARDHI YA MWANZA



Ali Kiba, Diamond Platnumz pamoja na Ben Paul wamehusishwa kwenye majibu ya maswali aliyoulizwa na waaandishi wa habari yaliyoelekezwa kwake mwanamuziki Papii Kocha wakati akitua kwa mara ya kwanza katika uwanja wa ndege jijini Mwanza.

Ndani ya abiria waliotua hii leo majira ya saa 5:20 asubuhi kwa kutumia ndege ya shirika la Precision Air,  yumo mwanamuziki Nguli wa muziki wa Dansi nchini Tanzania Nguza Viking al maarufu Babu Seya akiwa na mwanaye Papii Kocha ambao ujio wao unakuja  kwaajili ya kuikata ile kiu ya muda mrefu ya burudani ya muziki wa ukweli waliyoikosa kwa takribani miaka 14 wakazi wa Kanda ya Ziwa miji ya Mwanza na Geita.


 







 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.