ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, April 23, 2018

WAISLAMU KENYA WAKEMEA ONGEZEKO LA VITENDO VYA USHOGA NA USAGAJI KATI YA WANAFUNZI.

Wanafunzi nchini Kenya, ambao serikali imetakiwa kuwalinda kutokana na vitendo vichafu mashuleni
Waislamu visiwani Zanzibar wametakiwa kuienzi misikiti sambamba na kuifanyia usafi kila wakati. Kadhalika Waislamu wametakiwa kuzitumia nyumba hizo za Mwenyezi Mungu katika kukemea vitendo vya udhalilishaji dhidi ya wanawake na ulawiti.
Hayo yanajiri katika hali ambayo Baraza la Ushauri la Waislamu nchini Kenya, KEMNAC, limeitaka Wizara ya Elimu kwa kushirikiana na asasi za elimu nchini humo kukabiliana vikali na wimbi la vitendo vya ushoga na usagaji vinavyoshika kasi kati ya wanafunzi wa shule mbalimbali, suala ambalo linatishia mustakbali na vijana hao na taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa na Sheikh mwenyekiti wa baraza hilo Sheikh Juma Ngao ambaye amedokeza kwamba, akthari ya wanafunzi wamekumbwa na visa hivyo vya kuchukiza. Na katika sehemu nyingine Waislamu wametakiwa kuukaribisha mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kujipambana na akhlaqi za dini ya Kiislamu sambamba na kujiepusha na matendo ya maasi maarufu kwa jina la 'Vunja jungu' ambayo hufanywa siku ya mwisho kabla ya mwandamo wa mwezi huo mtukufu.
Mwezi wa Ramadhan ambao Waislamu wametakiwa kuupokea bila kufanya maasi
Hayo yameelezwa katika mimbari mbalimbali za swala ya leo ya Ijumaa ambapo pamoja na mambo mengine Waislamu wamekumbushwa juu ya ubaya na ukubwa wa dhambi ya kushiriki maasi katika kuukaribisha mwezi wa ibada wa Ramadhani. Na katika sehemu nyingine Waislamu wametakiwa kuacha kuitana majina mabaya na kukufurishana kwa sababu tu ya mwandomo wa mwezi huo na kwamba suala hilo linaweza kutatuliwa bila kukufurishana.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.