ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, April 25, 2018

RWANDA YAFUNGA RADIO YA KIKRISTO YA MAREKANI KWA KUCHOCHEA CHUKI.

Rwanda imeipokonya leseni kituo kimoja cha radio cha Kikristo kinachomilikiwa na Marekani, kwa kueneza chuki.
Mamlaka ya Kudhibiti Mawasiliano Rwanda (RURA) imeifunga idhaa ya Amazing Grace Christian Radio, kwa kukiuka kanuni za matangazo.
Katika taarifa iliyotolewa jana Jumanne, RURA imesema imeamua kufunga radio hiyo inayomilikiwa na Marekani kwa kushindwa kufuata maadili ya umma sanjari na kukiuka thamani na tamaduni za nchi hiyo ya Kiafrika.
Miezi miwili iliyopita, Mamlaka ya Kudhibiti Mawasiliano Rwanda ilisimamisha matangazo ya radio hiyo kwa muda wa mwezi mmoja, kwa kupeperusha vipindi vya kueneza chuki za kidini, mbali na kuwadhalilisha wanawake.
Rwanda kwa sasa inaadhimisha siku 100 za kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya 1994, yaliyochochewa pakubwa na radio
Mamlaka hiyo imeashiria kuwa, Januari 29 mwaka huu, mtangazaji mmoja wa Amazing Grace Christian Radio inayomilikiwa na Marekani aliwadhalilisha wanawake kwa kusema kuwa ni waovu, huku akizikashifu na kuzitupia cheche za maneno makali dini nyinginezo.
Rwanda na Marekani zimekuwa katika msuguano wa chini kwa chini katika miezi ya hivi karibuni, kwani mapema mwezi huu Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kusimamisha kwa muda usiojulikana mpango wa kutozitoza ushuru nguo zinazoingia nchini humo kutoka Rwanda, uliokuwa ukitekelezwa chini ya mpango wa African Growth and Opportunity.
Hatua hii ilijiri baada ya Rwanda kuongeza ushuru wa forodha uliokuwa ukitozwa nguo kuu kuu (mitumba) zinazoingizwa nchini humo kutoka Marekani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.