ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, April 22, 2018

RAIS WA SYRIA AKATAA TUZO.

Syria imerejesha kwa Ufaransa tuzo ya Légion d'honneur aliyopewa rais Bashar al-Assad, ikisema kuwa haiwezi kuchukua tuzo kwa taifa ambalo limekuwa 'mtumwa' wa Marekani.

Hatua hiyo inajiri siku moja baada ya Ufaransa kusema kuwa adhabu ya kuikataa tuzo hiyo inakaribia.

Ufaransa hivi majuzi ilijiunga na Ufaransa na Uingreza katika kuishambulia Syria kufuatia madai ya kutumia silaha za kinyuklia dhidi ya raia wake.

Tuzo hiyo ilirudishwa Ufaransa kupitia balozi ya Roma mjini Damascu

Rais Assad alipewa tuzo hiyo ya hadhi ya juu 2001 baada ya kuchukua mamlaka kufautia kifo cha babake.

''Wizara ya maswala ya kigeni imerudisha kwa Jamhuri ya Ufaransa tuzo ya Légion d'honneuri iliopewa rais Assad'', wizara ya kigeni nchini Syria ilisema katika taarifa.

''Sio heshima kwa rais Assad kuvaa tuzo iliotolewa na taifa la utumwa na mshiriki wa taifa la Marekani linalounga mkono ugaidi'', iliongoza.
Takriban watu 3,000 kila mwaka hutuzwa tuzo hiyo ya hadhi ya juu kwa huduma waliotoa kwa Ufaransa ama kwa kutetea haki za kibinaadamu, uhuru wa kujieleza ama sababu kama hizo.

Marekani , Uingereza na Ufaransa zilishambulia vifaa kadhaa vya serikali ya Syria siku ya Jumamosi ili kujibu matumizi ya silaha za kemikali katika mji wa Douma, ambao ndio mji wa mwisho uliokuwa ukikaliwa na waasi katika jimbo la mashariki mwa Ghouta nje ya Damascus.

Zaidi ya watu 40 walifariki katika shambulio hilo la Aprili 7 kulingana na wanaharakati wa upinzani, wafanyikazi wa uokoaji na maafisa wa matibabu.

Serikali ya Syria imekana kutumia silaha za kemikali na kusema kuwa shambulio hilo lilipangwa.

Viongozi wengine waliopokezwa tuzo hiyo ni pamoja na aliyekuwa rais wa Tunisia Zine El Abiine Ben Ali 1989 na rais wa Urusi Vladimir Putin 2006.

Kufikia sasa ni rais mmoja pekee aliyepokonywa taji hilo-rais wa Panama Manuel Norriega. Hivi majuzi Nyota wa Hollywood Harvey Weinstein pia alipokonywa tuzo hiyo baada ya kukabiliwa na mashtaka ya unyanyasaji wa kingono.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.