ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 7, 2018

KUTOA HAKI SAWA KWA WOTE NDIYO MSINGI MKUU WA MAHAKAMA NCHINI TANZANIA


KATIKA kufikia malengo ya utoaji Haki sawa kwa wote na kwa wakati Mahakama ya Tanzania kupitia Kanda zake nchini, imeendesha mafunzo kwa watendaji wake wa vitengo mbalimbali.

Mkoani Mwanza Mkutano wa kujadili mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania 2015 – 2020 umefanyika ijumaa hii ya Tarehe 6 April 2018 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Mkuu wa mkoa wa Mwanza aliopo wilayani Nyamagana ukijumuisha wadau wa Mahakama kutoka wilaya mbili za Ilemela na Nyamagana pamoja na Mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Mwanza.

Licha ya kuwa na changamoto ya uhaba wa vifaa na watumishi Mahakama nchini Tanzania imeendelea na ujenzi na uboreshaji wa Mahakama zake za Mwanzo,Wilaya na hata zile za  Mkoa na hivi karibuni ujenzi utakamilika nao mkoa wa Mara kukabidhiwa Mahakama Kuu ya Kanda.

"Kwahiyo itapunguza gharama na usumbufu wa ule umbali wa mtu kusafiri mwendo mrefu kuja mkoani Mwanza kwaajili ya kusikilizwa shauri lake" Alisema Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe. Robert Vicent. CHEKI VIDEO.

Mkutano huo wa mafunzo umeandaliwa na Ofisi ya hakimu Mkazi mfawidhi mkoa wa Mwanza ambapo Watoa maada au wawezeshaji wakiwa ni Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi mkoa wa Mwanza Mh Wilbert M.Chuma na Mtendaji wa Mahakama kuu Moses Minga.

"Mafunzo hayo ni endelevu na tunatarajia kuendesha pia mafunzo hayo kwa wilaya zilizobaki ndani ya mkoa wa Mwanza  kama vile Magu , Sengerema , Misungwi  , Ngudu Kwimba na Ukerewe lengo likiwa ni kuhakikisha kila mtumishi anauishi mpango mkakati husika" Alisema Mhe. Chuma.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.