ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, April 6, 2018

HAYA NDIYO YALIYOJITOKEZA KWENYE MKUTANO WA KUJADILI MPANGO MKAKATI WA MAHAKAMA YA TANZANIA 2015-2020 JIJINI MWANZA

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe. Robert Vicent ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mkutano huo.
KATIKA kufikia malengo ya utoaji Haki sawa kwa wote na kwa wakati Mahakama ya Tanzania kupitia Kanda zake nchini, imeendesha mafunzo kwa watendaji wake wa vitengo mbalimbali.


Mkoani Mwanza Mkutano wa kujadili mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania 2015 – 2020 umefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Mkuu wa mkoa wa Mwanza aliopo wilayani Nyamagana ukijumuisha wadau wa Mahakama kutoka wilaya mbili za Ilemela na Nyamagana pamoja na Mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Mwanza.

Pia Mkutano huo umelenga kupitia mpango mkakati huo, kuujadili utekelezaji wake mpaka sasa, kubaini changamoto, mafanikio lakini pia na kuona nini kifanyike kwaajili ya kuendeleza na kutekeleza utoaji maamuzi ya haki na kwa umakini zaidi kwa manufaa ya wadau wanaohudumiwa.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe. Robert Vicent ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mkutano huo amewaasa washiriki hao kufanya kazi kwa weredi, kwa kuzingatia uwajibikaji, maadili, nidhamu huku wakitambua kuwa Serikali imewapa dhamana kubwa watumishi ngazi mbalimbali za mahakama  katika kuhakikisha kuwa haki inatendeka katika utoaji maamuzi.

Yote haya yamefanyika yakilenga dira ya Mahakama inayosema HAKI SAWA KWA WOTE NA KWA WAKATI.

Kwa mujibu wa Mhe. Robert, ni matarajio yake kwamba kila mdau wa Sheria atashiriki ipasavyo katika kutekeleza mpango uliowekwa kwenye mpango mkakati wa Mahakama kwa kuzingatia nguzo tatu muhimu za mpango mkakati huo ambazo amezitaja kuwa ni  pamoja na:- 
1.UTAWALA BORA UWAJIBIKAJI NA USIMAMIZI WA RASILIMALI.
2.UPATIKANAJI NA UTOAJI HAKI KWA WAKATI.
3.KUIMARISHA IMANI YA JAMII NA USHIRIKISHWAJI WA WADAU KATIKA SHUGHULI ZA MAHAKAMA.

MATEGEMEO
Baada ya Mkutano na Majadiliano yake kila mmoja atatekeleza  mpango huo kwa uadilifu, uwajibikaji, uwazi pamoja na kuzingatia weredi.

Mkutano huu wa mafunzo umeandaliwa na Ofisi ya hakimu Mkazi mfawidhi mkoa wa Mwanza ambapo Watoa maada au wawezeshaji wakiwa ni Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi mkoa wa Mwanza Mh Wilbert M.Chuma na Mtendaji wa Mahakama kuu Moses Minga.


"Mafunzo hayo ni endelevu na tunatarajia kuendesha pia mafunzo hayo kwa wilaya zilizobaki ndani ya mkoa wa Mwanza  kama vile Magu , Sengerema , Misungwi  , Ngudu Kwimba na Ukerewe lengo likiwa ni kuhakikisha kila mtumishi anauishi mpango mkakati husika" Alisema Mhe. Chuma.

Jumla ya washiriki 68 wamehudhuria Mkutano huo ambao ni Mahakimu, Makarani, Wahudumu wa Mahakama pamoja na Madereva.
















Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.