ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, April 30, 2018

AMUUWA MPENZI WAKE KWA KUMNYONGA.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia kijana aliyefahamika kwa jina la Nicholas Light (25) mkazi wa Mtaa wa Mahama Ilemela kwa kunyonga mpenzi wake Victoria Swai (26).

Inadaiwa kijana huyo alifanya mauaji hayo kwa kumkaba shingo mpenzi wake huyo hali iliyopelekea kukosa hewa na baadae kufariki dunia.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kudai tukio hilo limetokea katika jengo la Ekacliff ofisi ya Kilimanjaro Avitaion.

Katika tukio hilo polisi walifanya uchunguzi katika nyumba alipokuwa akiishi marehemu na mpenzi wake na kumkuta mtuhumiwa akiwa amejificha juu ya dari ya nyumba.

Chanzo cha mauaji hayo kinadaiwa kuwa ni  wivu wa kimapenzi ambapo mtuhumiwa huyo  alikuwa akimtuhumu marehemu kuwa alikuwa akimsaliti kimapenzi ambapo  mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa ajili ya uchunguzi zaidi, pindi uchunguzi ukikamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.