ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 26, 2018

SHIRIKA LA NDEGE LA WATANZANIA WOTE. FASTJET, KUANZIA LEO LINARAHISISHA ZAIDI USAFIRI WA ANGA KWA KUPUNGU BEI ZA MIZIGO KWA KUUZA NUSU BEI.


Fastjet yatoa ofa ya abiria kusafiri na kila mzigo kwa nusu bei, Shirika la ndege la kila mtanzania laendelea kutoa usafiri wa anga ambao kila mtu anaweza kuumudu. Nunua tiketi mapema na uokoe pesa.

Dar es salaam: Shirika la ndege la watanzania wote, Fastjet, kuanzia leo linarahisisha zaidi usafiri wa anga kwa kupunguza bei za mizigo kwa kuuza nusu bei. Kila begi la kuingia chini ya ndege sasa litauzwa tsh 22,000 unaweza kulipia mzigo wako wakati wa kununua tiketi na Tsh 44000 unapolipia uwanja wa ndege muda wa safari safari. Bei hii inapatikana kwa abiria wote wanaokata tiketi kuanzia leo hadi tarehe 30 Juni. Unaporuka na Fastjet daima unajihakikishia nauli utakayoimudu na kupaa na kutua kwa wakati, kwa punguzo hili la bei kwenye mizigo linafanya safari yako kuwa rahisi zaidi.

 “Upatikanaji wa huduma ya usafiri wa anga ambayo kila mtu anaweza kuimudu ni muhimu sana kwa shirika letu la fastjet” alisema msemaji wa Fastjet Lucy Mbogoro. “Bei hizi mpya zilizopunguzwa zinatoa pia unafuu kwa wafanyabiashara kubeba mizigo yao kwa  kwa bei nafuu zaidi, hivyo kutoa fursa za kimaendeleo kwa wote.” Mbogoro aliongeza kuwa shirika pia linafanya juhudi kuboresha huduma kwa wateja “Tunafanya kazi kwa juhudi sana kuhakikisha kila hatua anayopitia mteja wetu inampa tabasamu na hii tayari inaonekana katika Matokeo yetu ya kuondoka na kufika kwa wakati kwa mwezi Januari na Februari ambapo Fastjet ilizidi 90% kwa miezi yote”

Bei hii ya mizigo iliyopunguzwa inapatikana kwa safari za Fastjet kati ya Dar es Salaam na Mwanza, Dar es Salaam na Mbeya na Dar es Salaam na Kilimanjaro. Mbogoro aliongeza kwa kutoa dondoo ya safari “Ni rahisi kuokoa pesa unaposafir na Fastjet kwa kukata tiketi mapema.” Hivyo alisema  “Unapoandaa safari yako mapema na kukata tiket mapema unapata fursa ya kuokoa pesa.” Bei zetu za kila mzigo kwa tsh 22,000 zinaanza rasmi tarehe 2 Machi 2018.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.