ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, March 22, 2018

MMILIKI WA FACEBOOL AWAOMBA RADHI WATUMIAJI WA MTANDAO WAKE.

Mkurugenzi Mkuu na mmliki wa mtandao wa kijamii wa Facebook Mark Zuckerberg amevunja ukimya juma hili kuhusu kashfa iliyoikumba kampuni yake ambapo ameomba radhi kutokana na "kuvunja uaminifu" kwa weteja wake zaidi ya bilioni moja na kuapa kutorudia makosa yaliyojitokeza.
Katika matamshi yake ya kwanza kwa umma kuhusiana na matumizi mabaya ya taarifa binafsi za wateja zaidi ya milioni 50 kulikofanywa na kampuni ya Uingereza iliyokuwa na uhusiano na timu ya kampeni ya Rais Donald Trump mwaka 2016, Zuckerberg amewaambia watumiaji wa Facebook kuwa taasisi yake "ilikuwa na wajibu wa kulinda taarifa zao."
Ameahidi pia kuwa Facebook itachunguza kila programu iliyopata mwanya wa kupitia akaunti za wateja wake na kufanya uchunguzi wa kisayansi kwa kitu chochote kilichoonekana kina wasiwasi.
"Huu ulikuwa ni uvunjifu mkubwa wa matumizi ya taarifa binafsi na uaminifu, nawaomba msamaha kwa kile kilichotokea," alisema Zuckerberg wakati akihojiwa na kituo cha televisheni cha CNN.
Imebainika kuwa kampuni ya Uingereza Cambridge Analytica ilifanikiwa kudukua taarifa binafsi za mamilioni ya watumiaji wa mtandao wa kijamii wa Facbook kupitia progarmu maalumu ya utafiti uliofanywa na Aleksander Kogan na ambayo ilipakuliwa na mamilioni ya watumiaji wa mtandao huo na kuchukua taarifa za marafiki wengine.
"Hiki kilikuwa kitendo cha uvunjifu wa uaminifu kati ya Kogan, Cambridge Analytica na Facebook," aliandika Zuckerberg. "Lakini ni kuvunja uaminifu kati ya Facebook na watu ambao wametoa taarifa zao kwetu na walitarajia tuzilinde."

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.