ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 24, 2018

KUHUSU TAARIFA ZA KUFUNGIA MITANDAO YA KIJAMII, SERIKALI YAFUNGUKA HAYA.

Kumekuwa na uvumi unaosambazwa katika mitandao ya kijamii kutoka kitengo cha Rais, Ikulu idara ya Mawasiliano ikidai kuwa, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imearifu wananchi wake kufungia mitandao ya kijamii nchini endapo itatumika vibaya.

Kufuatia habari hiyo ambayo hata hivyo inaonesha ni ya mwaka 2017,  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais- Ikulu, Gerson Msigwa mapema leo hii ameikanusha barua hiyo na kudai kuwa haijachapishwa na idara yake.

Msigwa amewasihi Watanzania kuipuuza habari hiyo kwani ni uvumi ambao hauna ukweli wowote, kwani Serikali haijatoa wala kuzungumzia swala hilo.

Taarifa hii imetengenezwa na wahalifu wa mtandao. IPUUZWE. pic.twitter.com/frwWozW12U
— Gerson Msigwa (@MsigwaGerson) March 24, 2018


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.