ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, March 20, 2018

CHAMA CHA USHIRIKA CHA NYANZA KUFUFUKA KWA KASI MONGELA ATANGAZA VITA NA VIONGOZI WAPYA.



NA ZEPHANIA MANDIA 
MKUU wa mkoa wa Mwanza John Mongella amewatahadhalisha wajumbe wa zao la pamba kuepuka kuchagua viongozi wasio na sifa kwa kigezo cha kupewa rushwa.

Tahadhali hiyo ameitoa kwenye Mkutano Mkuu wa Chama Cha Ushirika Nyanza uliofanyika katika ukumbi wa chama hicho katikati ya jiji la Mwanza, huku kukiwa na agenda kadhaa ikiwemo uchaguzi wa viongozi na wajumbe wa bodi ya chama hicho.

"Nasikia wapo tuliowanyang'anya mali za Ushirika walizojimilikisha kwa mlango wa uwani, mara baada ya kujiuzia kwa pesa ndogo, za wizi wizi sasa wamefadhili baadhi ya watu miongoni mwenu kwa kuwapa fedha na nyinyi mnawajua"
 "Wametoa vihela vyao, wamevimwaga kwa wajumbe tunaowaamini na sasa wanataka kurudi kwenye madaraka watusumbue tena"

"Nataka kuwaambia kwamba tunawafahamu wakirudi mtaona, kwani hawatofika hata kesho, tutawafuta"
 WAKATI HUO HUO
Serikali imetakiwa kuendelea kutoa ushirikiano kwenye chama cha Ushirika cha Nyanza na kuweka mikakati thabiti ya kufufua zao la pamba na kulifanya kuwa la biashara ili kuweza kusaidia kendeleza ushirika huo wa Nyanza katika mkoa wa Mwanza.

Chama Cha Ushirika Nyanza kimewakutanisha wanachama wake kutoka mikoa mbalimbali ya Kanda ya Ziwa inayolima zao hilo ambayo ni MWANZA, GEITA NA SIMIYU, lengo kuu likiwa ni kujadili changamoto mbalimbali za zao la pamba na namna ya kuzipatia ufumbuzi.
 Hawa ni baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka kanda zinazolima zao la pamba nao wanaeleza nini imani yao kwa zao hilo ambalo kwa hivi sasa Serikali imeamua kulisimamia mguu kwa mguu. 







Akisoma taarifa ya Mwenyekiti wa Bodi ya Nyanza Simon Mbata ambaye ni mjumbe wa Bodi amewataka viongozi wa Kanda zinazolima zao hilo kuwa waadilifu katika ununuzi 

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella amesema kupitia Nyanza juhudi ziendelee kufanyika hata kulifufua zao hilo.

Kutokana na umaarufu wa zao la pamba wakulima wameamua kulipa jina la dhahabu nyeupe.

Kauli mbiu ya mkutano mkuu wa 26 wa Chama Chama Cha Ushirika Nyanza inasema Tanzania ya Viwanda Itawezekana kupitia vyama vya ushirika vya msingi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.