ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, February 20, 2018

WAENDESHA BAISKELI ZA ABIRIA WAPINGA AGIZO LA KUONDOKA MJINI GEITA

Baadhi ya waendesha Baiskeli maarufu kwa jina la dala dala wakiwa wamekusanyikana sehemu moja kujadili mustakabali wa kuondolewa kwenye maeneo ya mjini.

Waendesha Baskeli wakiwa maeneo ya mjini  Geita.


Waendesha Baiskeli wakitafakali juu ya hatua ya kuondolewa mjini Geita.

Na,Joel Maduka,Geita.
Waendesha Baiskeli Maarufu kwa jina la daladala wanaosafirisha abiria kwenye halmashauri ya mji wa Geita, wamepinga agizo la Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo la kuwataka kufikia leo wasitishe shughuli zao kwenye maeneo ya mjini badala yake wafanye kwenye maeneo waliyopangiwa.

Hatua hiyo imekuja baada ya kupewa muda wa siku tano kupisha maeneo ya mjini kutokana na wimbi la ajali zinazosababishwa na waendesha Baiskeli kwa kutotumia barabara vizuri wanapokuwa kwenye shughuli zao.

Baadhi ya waendesha Baiskeli hao Bw Vistusi Maagani, John Maige na Fredy Maganga wamesema utaratibu uliofanyika sio mzuri kwa kuwa hawajapewa maeneo yatakayowasaidia kufanya kazi zao .

“Nasikitishwa sanaa na kitendo cha Mkurugenzi kututoa bila ya kutuandalia maeneo mazuri ya kufanyia kazi zetu kwa mfano mimi hapa hii kazi ndio nategemea kulisha familia pia kutuma pesa kwa mama yangu mzazi kwa kuwa sina ndugu leo natolewa kufanya kazi mjini unategemea nitaishi maisha gani jamani na wale ambao wananitegemea nitawaelezaje mimi naomba haya maamuzi wayaangalie kwa umakini”Alisema Maagini.

“Nashindwa hata niseme nini najisikia moyo wangu kutoka  kabisa kutokana na taarifa hii ya kuondolewa mjini maeneo ambayo tunaambiwa kufanya kazi akuna abiria sasa sijui tutaishije sisi waendesha daladala”Alisema  Maganga.

Bi,Lucia Paul ambaye mume wake anajishughulisha na kazi hizo alisema  kuondolewa mjini kwa waendasha baiskeli kutaleta athari kwenye familia zao kutokana na wengi wao kutegemea shughuli hiyo kukidhi mahitaji ya familia.

“Kwasasa hivi nyumbani hapakaliki kila siku mume wangu anamawazo anashindwa afanye nini na uku anafamilia muda mwingine hadi namuonea huruma  serikali ni vyema ikaangalia maana itatupa wakati mgumu sisi wanawake ambao tunawategemea waume zetu kwenye utafutaji”Alisisitiza Lucia.

Kutokana na hali hiyo chama cha ACT wazalendo kupitia kwa katibu wa mkoa huo,Bw Ikolongo Otoo  ameitaka halmashauri ya mji wa Geita kuondoa mara moja zuio hilo  kwa kuwa ni la kibaguzi ambalo alijazingatia wala kuthamini vijana masikini na wanyonge ambao wameamua kujipatia vipato kwa njia halali kabisa.

Mkurugenzi wa Halmashari ya mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinaly  alisema suala ambalo linafanyika ni la utekelezaji na alilikuwa aliitaji  muda kwani maeneo ambayo wamewapatia kufanya biashara ni makubwa na kwamba hata wangepewa muda  wa kutosha bado wangeombwa kuongezewa.

Mbunge wa Jimbo la Geita mjini,Constatine Kanyasu alisema  ahafikiani na makubaliano hayo na kwamba akuna utaratibu wala sheria ambayo inawazuhia waendesha Baiskeli kufanya shughulo zao maeneo ya mjini.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.