ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, February 15, 2018

KIJANA WA MIAKA 19 AWAPIGA RISASI NA KUWAUA WATU 17 KATIKA SHULE MOJA YA SEKONDARI NCHINI MAREKANI.

 
WATU wasiopungua 17 wameuawa na makumi ya wengine wamejeruhiwa baada ya kijana mmoja mwenye umri wa miaka 19 kufyatua risasi katika skuli moja ya sekondari ya eneo la Parkland katika jimbo la Florida nchini Marekani.


Kwa mujibu wa polisi, muuaji huyo ambaye ameshakamtawa na ambaye amejulikana kwa jina la Nikolaus Cruz, alikuwa mwanafunzi wa zamani wa shule hiyo lakini alifukuzwa kwa sababu ambazo hazijabainishwa za utovu wa nidhamu.
Cruz.
Ripoti ya Polisi imeeleza kuwa katika tukio hilo lililojiri hapo jana, Cruz kwanza alianza kufyatua risasi kutokea nje ya skuli kabla ya kuingia ndani na kuanza kuwafyatulia risasi wanafunzi wa skuli hiyo ya Marjory Stoneman Douglas.
Maafisa wa hospitali katika jimbo la Florida wamesema hadi sasa watu 17 wamethibitika kuwa wameuawa na wengine 20 hadi 50 wamejeruhiwa, ambapo hali za baadhi ya majeruhi ni mahututi.

 Watu wakitolewa nje ya eneo la shule ya Marjory Stoneman Douglas baada ya mauaji hayo kutokea huku wengine wakijeruhiwa. (Photo by Joe Raedle/Getty Images)
 Rais Donald Trump wa Marekani, ambaye yeye mwenyewe ni muungaji mkono wa sera ya uhuru wa kumiliki silaha nchini Marekani amesema kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Twitter kuwa: haipasi mtu yeyote ajihisi hana usalama katika skuli za Marekani.


Kila mwaka maelfu ya watu huuawa na kujeruhiwa katika maeneo mbalimbali nchini Marekani katika matukio mbalimbali ya ufyatuaji risasi. Kwa mujibu wa ripoti rasmi kuna karibu silaha moto za mkononi milioni 270 hadi milioni 300 nchini Marekani, ikiwa na maana kwamba, kwa wastani kuna silaha moja moto kwa kila raia mmoja wa nchi hiyo.
Licha ya miito inayoendelea kutolewa kila leo na makundi ya kutetea haki za kiraia nchini Marekani, lakini kutokana na ushawishi wa lobi za viwanda vya utengezaji silaha, hakuna serikali yoyote ya nchi hiyo ambayo hadi sasa imeweza kutunga sheria ya kudhibiti uuzaji silaha kwa raia nchini humo.

Kikosi cha zimamoto na uokoaji kikiwa eneo la tukio kutoa msaada. (Photo by Joe Raedle/Getty Images)

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.