ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 23, 2018

ADO SHAIBU KATIBU MWENEZI ACT WAZALENDO AZUNGUMZIA KILICHOTOKEA KWA ZITTO KABWE



Baada ya Kiongozi Mkuu wa Chama Cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe kukamatwa na Polisi na kuwekwa ndani wakati akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika kata ambazo Chama hicho kinaongoza. 

Jembe Fm kupitia kipindi chake KAZI NA NGOMA kimemtafuta kwa njia ya simu Katibu Mwenezi wa chama hicho, ADO SHAIBU naye amezungumza kile kilichomtokea Mhe. Zitto, huku akijinadi kwa kusema, kwa hatua hiyo hawatorudishwa nyuma.

BAADA YA KUTOKA ZITTO AZUNGUMZA HAYA.
Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo amefunguka na kuwataka watu wasirudishwe nyuma kwa vitisho na usumbufu wa sheria kandamizi zinazopelekea baadhi ya viongozi kukamatwa na kuwekwa ndani.

Zitto Kabwe ameweka wazi hayo mara baada ya kuachiwa leo Februari 23, 2018 na kusema kuwa yeye anaendelea na harakati zake ya kuwafikia viongozi na Kata ambazo wananchi waliwachagua viongozi wa ACT Wazalendo.

"Tusirudishwe nyuma na vitisho, usumbufu na sheria kandamizi. Harakati za kulinda Demokrasia yetu na Uhuru wa kukusanyika, kujieleza na kupashana habari lazima ziendelee. Ni wajibu wetu kulinda Demokrasia ya Vyama vingi na kuiimarisha iwe madhubuti kwa ajili ya Maendeleo ya Watu wetu. Baada ya kulala bure jana polisi Morogoro, tunaendelea na kazi yetu ya kutembelea kata zote ambazo Wananchi walitupa dhamana kwa kuchagua madiwani wa Act Wazalendo" alisema Zitto Kabwe

Aidha Zitto Kabwe ameonyesha kuguswa na muaji mengine ambayo yametokea jana ambapo diwani wa CHADEMA ameauwa kwa kukatwa mapanga sehemu mbalimbali katika mwili wake

"Nawapa pole Wananchi wa Ifakara kwa msiba wa Diwani wao aliyekatwa mapanga mpaka kufa jana Usiku. Nilipata taarifa hizo nikiwa selo ya Polisi. Mauaji ya namna hii kwa Viongozi wa kisiasa yanatia doa nchi yetu na ni mwendelezo ya uvunjifu mkubwa wa haki za raia" alisema Zitto Kabwe

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.