ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, January 26, 2018

LUKUVI AJA NA MAAMUZI HAYA JIJINI MWANZA

WANANCHI wanaomiliki nyumba 664 katika mitaa ya Kigoto na Kabuhoro katika Kata ya Kirumba Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza wametakiwa kuwa na subira wakati serikali ikitafuta ufumbuzi wa mgogoro uliopo kati yao na Jeshi la Polisi.

Pia wamezuiwa kujenga nyumba nyingine mpya kwenye maeneo ya mitaa yao na badala yake wawe walinzi na kuonya watakaothubutu kujenga hawatalipwa fidia ambapo awali walitakiwa kuondoka na kupisha eneo hilo baada ya kuandikiwa ilani ya siku saba na jeshi la polisi.

Akizungumza na wananchi hao Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alisema serikali imesikia kilio chao na hivyo amekuja chunguza mgogoro huo ili ifanye uamuzi wa kuutatua.

 Amesema serikali inataka kufahamu mahitaji ya wananchi na polisi na kuonya wananchi wanaoishi kwenye maeneo hayo wasithubutu kujenga (kuongeza) majengo mengine zaidi ya yaliyopo sasa na watakaokaidi hawatalipwa fidia.

“Nimekuja kuangalia mgogoro huu na kuchungumza jambo hili ili serikali ifanye uamuzi. Msidhani nina majibu, majibu yatatolewa ndani ya mwaka mmoja lakini msituhubutu kuongeza nyumba zingine zaidi, kuweni walinzi wa maeneo haya na tunataka muwe maeneo mzuri ili tuwarasimishie,”alisema Lukuvi.

Waziri huyo wa ardhi alisisitiza baada ya uchunguzi atamshauri vizuri Rais John Magufuli namna ya kumaliza mgogoro huo baina ya wananchi na taasisi hiyo ya serikali.

Lukuvi alieleza eneo la Kigoto ambalo Polisi inadai inataka kujenga Chuo cha Polisi wanamaji, nyumba za askari, gati la boti na meli za doria zinaweza kujengwa popote lakini eneo hilo lazima lipangwe upya hata kama matumizi yakibadilishwa kwa kuwa haiwezekani watu waishi kwenye nyumba za hoovyo hovyo.

“Miaka 70 hadi leo kwa nini ujenzi haukuzuiwa,hakuna viongozi hapa na kama mngewashirikisha wangewasaidia kuzuia.Je, upembuzi yakinifu ulifanyika kwenye eneo mnalotaka kujenga mdomo huo wa gati la boti za polisi?

Aidha akizungumza kwa niaba ya wenzao ,Ferdinand Mtundubalo alimweleza Waziri kuwa hawana tatizo na ujenzi wa gati la boti za polisi isipokuwa warasimishiwe makazi yao ili waondokanane na mgogoro huo.

Katika hatua nyingine Waziri Lukuvi aliwataka wataalamu wa wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela waainishe eneo la Uwanja wa Ndege wa Mwanza na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikosi cha Ihale ili kila mmoja alinde eneo lake.

Pia alishauri eneo la Nyamwilolelwa litakalobaki baada ya kutengwa la uwanja wa ndege na JWTZ lipimwe wapewe wananchi wa eneo wapatao 1,961 na kuhusu barabara ya Mwanza –Igombe uamuzi wa Rais Magufuli ubaki ulivyo na uheshimiwe.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.