ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 22, 2017

MAMA SALMA KIKWETE KUZINDUA KAMPENI YA KAMBI YA WANAFUNZI WA MASOMO YA SAYANSI MKOANI IRINGA




Wanafunzi wa shule za sekondari manispaa ya iringa kunufaika na elimu ya masomo ya sayansi kutokana na kuandaliwa kambi maalumu kwa ajili ya kuwafindisha kutoka kwa walimu waliobobea katika masomo hayo kwa wanafunzi wa watakao kuwa tayari kupata elimu hiyo.

Ofisi ya mbunge wa viti maalum Ritta Kabati imeandaa mpango wa kuwaongezea elimua wanafunzi wa shule za sekondari manispaa ya Iringa kwa kuanzisha kambi ya masomo ya sanyasi itakayo kuwa inafanyika bure kwa wanafunzi wa watakao kuwa tayari kupata elimu hiyo.

Akizungumza na Nuru fm Dicksoni Kawovela ambaye ni mratibu wa miradi ya jamii kutoka ofisi ya mbunge RITTA KABATI amesema kuwa wameamua kuja na mpango huo kwa lengo la kuinua elimu ya sayansi kwa wanafunzzi wa shule za sekondari hapa manispaa.

Aidha Kawovela amesema kuwa mafunzo hayo yatakuwa na manufaa kwa walimu na wanafunzi watakaokuwa wanahudhuria masomo haya ambayo yatakuwa yanatolewa bure.

Kawovela amewaka wazazi wa wanafunzi kuwaruhusu watoto wao kwenda kwenye makambi hayo ili waongezewe uwezo katika masomo ya sayansi.

Hata hiyo Kawovela alisema kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakuwa mama Salma Kikwete ambaye ni mbunge wa kuteuliwa na Rais katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MKUU WA JESHI LA POLISI, IGP SIMON SIRRO AFANYA ZIARA YA KIKAZI MKOANI LINDI KWA AJILI YA KUONGEA NA ASKARI.

 IGP Simon Sirro  akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Mkoa  ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mh Shaibu Ndemanga baada ya kuwasili mkoani Lindi katika ziara ya siku moja ya kuongea na Askari.  Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro wa tatu kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Lindi, kulia kwa IGP Sirro ni Kaimu Mkuu wa Mkoa  Mh Shaibu Ndamanga na kushoto kwake ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi Renata Mzinga.  Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (katikati) akiwa na Askari wa Mkoa wa Lindi baada ya kumaliza kukagua  mazoezi ya ukakamavu na utayari yaliokuwa yameandaliwa na kikosi cha kupambana na uhalifu mkoani  humo.  Picha na Jeshi la Polisi.

Thursday, December 21, 2017

ANTU MANDOZA KUTIMIZA NDOTO YAKE YA KUIGIZA NA RAMSEY NOAH KUTOKA NCHINI NIGERIA

 
 Antu Mandoza akiwa katika picha ya pamoja na Muigizaji nyota wa Filamu kutoka nchini Nigeria Ramsey Noah wakiwa katika picha ya pamoja.
Mwigizaji nyota wa filamu na Mkongwe wa tasnia hiyo kutoka nchini Nigeria ,Ramsey Noah ametamani kufanya kazi na nyota mwingine wa movie anaechipukia kwa kasi katika tasnia hiyo hapa nchini,ambae ameng'ara vilivyo katika filamu ya 'KIUMENI' , Antu Mandoza wa Tanzania . 
"Anaonekana ni binti mweye kipaji,anaejiamini,kwa hakika natamani nipate muda wa kubaini kipaji chake zaidi kwa kufanya nae angalau hata filamu moja,itaweza kumsaidia zaidi kujitanua na kutambulika Kimataifa",alisema Ramsey huku akimtazama Antu kwa tabasamu laini la ucheshi.

Antu Mandoza ni Binti wa makamo hivi,lakini amejaaliwa kuwa na kipaji cha uigiza wa filamu na mwenye uthubutu wa kufanya jambo.Antu Mandoza na Ramsey Noah walikutana katika Warsha fupi iliyoandaliwa na Sahara Group iliyofanyika hotel ya Hyatt Dar Es Salaam mnamo Desemba 16 2016,ambayo pia iliwahusisha wasanii mbali mbali wa bongo movie .

 Ikiwa ni movie yake ya kwanza 'KIUMENI', Antu Mandoza amefunguka na kusema kuwa mwaka ujao utakua ni mwaka wa kazi tu, kama ilivyo Slogan ya Raisi Dkt John Pombe Magufuli,na anategemea kufanya kazi na Ramsey Noah na wasanii wengine wengi wa Ndani na Nje ya Tanzania. 

Antu alijipatia Umaarufu katika filamu ya Kiumeni aliyocheza na Ernest Napoleon,ambayo lishinda tuzo 2 ZIFF mwaka 2017.

KIWANDA CHA POMBE BANDIA CHA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI MWNZA CHANASWA


Wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihimiza ulipaji wa kodi wapo wahujumu uchumi na wanaotumia vibaya Sera ya Tanzania ya viwanda.

Kupitia oparesheni iliyofanyika nyakati za usiku, Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limefanikiwa kubaini Kiwanda cha pombe bandia, watuhumiwa wa 4 huku wengine idadi isiyojulikana wakifanikiwa kutoroka.

Licha ya kiwanda hicho kutokuwa na leseni pia boksi za kutosha za stika za Mamlaka ya Mapato Tanzania  TRA  zimenaswa kiwandani  hapo. 

Wednesday, December 20, 2017

TFDA WANASA KAMPUNI LINALOZALISHA BIDHAA FEKI ZA KAMPUNI NYINGINE KWAAJILI YA KUHARIBU SOKO



Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA Kanda ya Kaskazini imekifungia kwa muda kiwanda cha GDT Company Factory Limited kinachozalisha vinywaji vya High Life Gin na Banana kwa kosa la kuzalisha bidhaa chini ya kiwango.

Pia kiwanda hicho kimekutwa na kosa la kujipatia faida kwa njia ya wizi kwa kuzalisha kinywaji aina ya #Shujaa ambacho ni mali ya kampuni nyingine, kinywaji ambacho kwa siku za hivi karibuni kimekuwa kikilalamikiwa na wateja wake kwamba kinaumiza kichwa.... Suala ambalo linasadikik kuwa limekuja mara baada ya mchezo huo mchafu. #HabariZilizoTikisa

VIDEO : RITTA KABATI KUKARABATI SHULE YA MSINGI KIHESA

 Na Fredy Mgunda,Iringa.




Mbunge wa viti maalam mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati amefanya ziara kwenye baadhi ya shule za msingi za manispaa ya Iringa kwa lengo la kubaini changamoto zilizopo na kuanza kuzitafutia ufumbuzi kwa lengo la kuboresha mazingira ya wanafunzi kusomea.



Akizungumza mara baada ya kumaliza zira hiyo ya wiki moja Kabati alisema kuwa amefanya ziara katika shule ya msingi Kihesa,Igereke,Mtwira na shule ya Kibwabwa na kubaini changamoto nyingi ambazo anaanza kuzitafutia ufumbuzi hivi karibuni.



“Nimejionea mwenyewe changamoto zilizopo na naona kama changamoto kwa asilimia kubwa zinafanana hivyo ni kazi yangu kuanza kutafuta njia ya kuanza kuzitatua changamoto hizo”alisema Kabati.

ADAM KIMBISA ABWAGWA U-SPIKA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI.


Bunge la Afrika Mashariki (Eala) limemchagua Spika kutoka Rwanda, Dk Martin Ngoga katika uchaguzi ulioibua mabishano ya kisheria juu ya uhalali wa kufanyika kwake.

Baada ya dua ya kuliombea Bunge, mbunge Dk Ngwaru Maghembe kutoka Tanzania aliomba mwongozo wa kuliahirisha kutokana na akidi kutotimia kutokana na wabunge tisa wa Burundi na saba wa Tanzania kutokuwepo kwa sababu ambazo hazikujulikana.

Mbunge kutoka Uganda, Freddy Mbidde alipinga hoja hiyo akisema kanuni ya 53(1) inayozungumzia akidi inahusu Bunge rasmi ambalo tayari lina Spika lakini kwa kuwa hawakuwa na Spika kanuni hiyo haina nguvu kisheria.

Mbunge mwingine wa Tanzania, Dk Abdullah Makame alisema kutokana na Bunge kuchelewa kuanza kazi kwa kipindi cha miezi sita kutokana na mwanachama wa EAC nchi ya Kenya kuchelewa kuchagua wabunge ni busara uchaguzi usifanyike hadi wabunge wote wawepo.

Hoja hiyo ilipingwa na mbunge kutoka Uganda, Suzane Nakauki aliyedai hoja ya kutokufanya uchaguzi kwa sababu ya wabunge kutokuwepo haina mashiko kisheria na kikanuni kwa sababu wameorodhesha majina yao kwenye kitabu cha mahudhurio na wamepewa posho na wameamua kwa sababu zisizojulikana kugomea uchaguzi.

Alisema haiwezekani wabunge wa Tanzania ambao wapo nchi mwao washindwe kuhudhuria kikao cha Bunge wakati wapo jijini Arusha, huku waliotoka mbali wakiwepo.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Balozi Liberat Mfumukeko alisema kila jambo lenye mgogoro kwenye mihimili ya EAC lina utaratibu wa kulimaliza kwa njia ya kuomba ushauri kwa sekretariati, Mahakama, baraza la mawaziri na kikao cha marais.

Hatua hiyo ilimwinua Waziri wa Afrika Mashariki wa Burundi, Isabella Ndahayo aliyesema wabunge wa Burundi hawakuridhishwa na utaratibu wa uchaguzi licha ya kanuni kutamka wazi nafasi ya Spika ni ya mzunguko kwa nchi wanachama.

"Wabunge wa Burundi hawapo kwa sababu hawaridhiki na kinachoendelea, naomba tupewe tafsiri ya nafasi ya Spika kuwa ni mzunguko kwa nchi wanachama, si kwamba tunapinga juhudi za mshikamano wa jumuiya bali tafsiri halisi," alisema Isabella.

Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Uganda ambayo ni Mwenyekiti wa EAC, Julius Wandera alisema kumekuwa na mashauriano kati ya baraza la mawaziri wa jumuiya hiyo ili kuhakikisha suala hilo linakamilika.

Baada ya mabishano ya kisheria na kanuni, katibu wa bunge aliamua uchaguzi kufanyika na awamu ya kwanza, mgombea kutoka Rwanda, Dk Martin Ngoga alipata kura 35, Leontine Nzeyimana wa Burundi kura moja na Adam Kimbisa wa Tanzania hakupata kura.

Kutokana na kanuni kuhitaji mshindi kupata theluthi mbili ya kura zote 52, uchaguzi ulirudiwa kwa kanuni ya mshindi kupatikana kwa wingi wa kura na Dk Ngoga aliibuka mshindi  kwa kupata kura 33 dhidi kura tatu za Nzeyimana ambaye hakuwepo bungeni.

Baada ya kula kiapo Dk Ngoga ambaye alikuwa mwendesha mashtaka mkuu wa Rwanda alisema anafahamu uchaguzi wowote lazima uache majeraha lakini yupo tayari kushirikiana na kila mbunge kujenga jumuiya hiyo.

VIONGOZI WA KIJIJI CHA MSOSA WILAYANI KILOLO WAVULIWA MADARAKA KWA NGUVU

mtendaji wa kata ya Ruaha Mbuyuni Maiko Chabili akiwafafanulia jambo wananchi wa kijiji wakati wa mkutano wa hadhara ulikuwa na lengo la kuwafukuza kamati ya mipango na fedha ya kijiji kwa matumizi mabaya ya pesa zao
 Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha msosa kilichopo tarafa ya ruaha mbuyuni walihudhuria mkutano wa hadhara wa kijiji

Na Fredy Mgunda,Iringa.



Wananchi wa kijiji cha msosa kilichopo tarafa ya ruaha mbuyuni wameifukuza kamati ya mipango na fedha kwa tuhuma za kufanya ubadhilifu wa mali za kijiji na kuunda kamati mpya itakayoleta maendeleo katika kijiji hicho.

Wakizungumza wakati wa mkutano wa hadhara ulifanyika katika kijiji hicho wanachi waliutaka uongozi wa kamati hiyo kuachia ngazi kutokana na tuhuma zinazowakabili.

 Kwa upande wake mtendaji wa kata MAIKO CHABILI ameafiki kuvuliwa madaraka kwa viongozi wa kamati ya mipangano na fedha kutokana na tuhuma zinazowakabili.

Hata hivyo kamati ya mipango na fedha ya kijiji cha msosa walikubali kujiudhuru na kulipa pesa ambazo ilibaini kuwa walizitumia vibaya bila ruhusa ya wananchi.

TUME YA ARDHI KUANZISHA KANZIDATA YA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDHI

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya mipango ya matumizi ya Ardhi(NLUPC) Dkt. Stephen Nindi akifungua mkutano wa kikosi kazi kwa ajili ya mchakato wa uanzishwaji wa kanzidata ya mipango ya matumizi ya ardhi,Mjini Morogoro.

Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) ipo mbioni kuanzisha Kanzidata (Database) ya mipango ya matumizi ya ardhi iliyofanyika nchini na wadau mbalimbali wa sekta ya ardhi.


Kwa kushirikiana na wadau wa upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi wa taasisi za serikali pamoja na asasi za kiraia, Kanzidata hiyo itabeba taarifa zitakazoonyesha maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali kama vile kilimo, malisho, huduma za jamiii, n.k itarahisisha utendaji kazi kwa Tume, mamlaka zingine za upangaji, wadau pamoja na wananchi kwa ujumla ambao watatumia teknolojia kujua maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali nchi nzima

Mwenyekiti wa Kikao Bw. Jamboi Baramayegu kutoka ujamaa Community akielezea utaratibu wa namna kazi itakavyofanyika
Afisa Tehama kutoka wakala wa Serikali Mtandao Bw. Thomas Malinga akitoa maelezo ya malengo ya wao kushiriki katika mchakato wa uanzishwaji wa uanzishwaji wa kanzi data ya mipango na matumizi ya ardhi.
Afisa Mipango wa Tume ya Taifa ya mipango ya matumizi ya Ardhi Bw. Gelard Mwakipesile, akielezea kwa kina kwa wajumbe wa mkutano kuhusu mipango ya matumizi ya ardhi,mchakato ulipo anzia hadi kuanza kwa  mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data ya mipango ya matumizi ya ardhi
 Bw. Paulo Tarimo kutoka Wizara ya Kilimo akichangia jambo wakati wa kikao cha mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data ya mipango ya matumizi ya ardhi.
 Baadhi ya wanakikosi kazi kutoka sekta mbalimbali wakiendelea na majadiliano ya kutoa maoni yao juu ya kuandaa mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data ya mipango ya matumizi ya ardhi.
 Katibu Mkuu wa Chama cha wafugaji Tanzania Bw. Magembe Makoye akiwasilisha mapendekezo yao kwa ajili ya mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data ya mipango ya matumizi ya ardhi kutoka katika kundi la wafugaji
 Bw. Godfrey Massay Meneja utetezi kutoka LANDESA  akiwasilisha mapendekezo yao kwa ajili ya mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data ya mipango ya matumizi ya ardhi kutoka katika kundi la Kilimo
 Afisa Sheria kutoka NLUPC Bi. Devotha Selukele akichangia jambo wakati makundi mbalimbali wakiwasilisha maoni yao juu ya kanzi data
 Afisa programu kutoka Haki Ardhi Bw. Joseph Kiombola   akiwasilisha mapendekezo yao kwa ajili ya mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data ya mipango ya matumizi ya ardhi kutoka katika kundi la Asasi za Kiraia.
 Afisa wanyama pori (TAWA) Bw. Herman Nyanda   akiwasilisha mapendekezo yao kwa ajili ya mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data ya mipango ya matumizi ya ardhi kutoka katika kundi la Maliasili
 Afisa Mpelembaji kutoka TNRF Bw. Wilbard   akiwasilisha mapendekezo yao kwa ajili ya mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data ya mipango ya matumizi ya ardhi kutoka katika kundi la Utafiti
 Wadau wakiendelea na mkutano huo.
Picha na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa Tanzania

Tuesday, December 19, 2017

SIKIO LA KUFA AROBAINI ZA DAKTARI FEKI HOSPITALI YA MKOA WA MWANZA



Jeshi la polisi jijini mwanza linamshikilia mtu mmoja Joseph Mbagata mkazi wa Mabati jijini humo kwa tuhuma za kujifanya daktari na kuwaibia wagonjwa katika hospitali ya mkoa Sekoture.

KUELEKEA KRISMASI AJALI YA COASTER YAUA WATANO BUHONGWA JIJINI MWANZA


Jeshi la polisi linawashikilia madereva wawili kwa uchunguzi kuhusiana na chanzo cha ajali iliyosababisha vifo vya watu watano na kujeruhi wengine 11 katika eneo la buhongwa jijini Mwanza.

MANYANYA: BADILISHENI UZOEFU KATIKA MAGEUZI YA VIWANDA.

  Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh.Stella Manyanya(Mb), Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Elisante Ole Gabriel na Mkurugenzi Msaidizi wa Mifumo wa OR TAMISEMI Baltazari Kibola wakati wa Kikao hicho kwa njia ya Mtandao kwenye Ukumbi wa Mikutano wa TAMISEMI. (Picha na OR-TAMISEMI)
 Mh. Mhandisi Stella Manyanya akiwa anawasiliana wakati wa kikao hicho cha siku tatu
 Mkutano unaendelea na hapo wajumbe wakiwa wanasikiliza Maswali kutoka Mikoani.
Wajumbe kutokea katika Ukumbi wa Mikutano wa OR TAMISEMI, Wakiwa wanafatilia kwa karibu na kusikiliza kupitia Screen kubwa inayonekana kwa mbele maelezo na majadiliano kutoka Mikoa iliyoshiriki Kikao hicho cha siku tatu.

Manyanya: Badilishaneni Uzoefu Katika Mageuzi ya Viwanda.
Na. Atley Kuni – OR-TAMISEMI.
Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na uwekezaji Mh. Mhandisi Stella Manyanya amefungua kikao cha siku tatu mjini Dodoma kwa njia ya Mtandao (Video Conferece) huku  akiwataka wataalam katika ngazi ya Mikoa za Mamlaka za Serikali za Mitaa kutumia mwanya huo kubadilishana uzoefu lakini pia kuibua fursa zilizopo katika maeneo yao katika  uanzishwaji na uendelezaji wa viwanda vidogo, vyakati na vikubwa ifikapo 2025.

Akifungua kikao hicho Manyanya alisema, kupitia fursa ya Viongozi hao wa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kukutana kwa njia ya Mtandao kutawezesha wote kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu mikakati ya ujenzi wa Uchumi wa Viwanda kwakupena taarifa za kujua viwanda vilivyopo katika maeneo yao na maendeleo yake, lakini pia kujua maeneo yaliyotengwa mahususi kwaajili ya viwanda hivyo.

“Mkutano huu utatusaidia pia kupambanua mikakati ya kufufua viwanda vilivyokufa na namna nzuri ya kupata wawekezaji wapya” alisema Manyanya na kuongeza kwamba  lengo la mikutano hiyo nikuwa na mkakati endelevu yakujenga uwezo kwa watendaji wa Mikoa na Halmashauri kuhusu masuala ya sekta ya Viwanda, Biashara na uwekezaji.

Manyanya amesema katika awamu ya kwanza Wakala wa Usajili Biashara na Leseni (BRELA), watatoa mafunzo juu usajili wa Biashara, Miliki Ubunifu sambamba na ujenzi wa uchumi wa Viwanda kama falsafa ya Mh. Rais wa awamu ya tano inavyojiapambanua kuhusu suala zima la viwanda.

Manyanya ameongeza kuwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Seleman Jafo pamoja na Waziri mwenye dhamana na Viwanda, Biashara na uwekezaji Charles Mwijage, ni viongozi ambao kwa nafasi zao wameonesha nia ya dhati katika kuhakikisha azma iliyowekwa na Serikali ya awamu ya Tano inatimia.

Akihitimisha risala yake ya ufunguzi Mh. Manyanya alisema, Mikutano hiyo ni mwanzo tu, kwani wanatarajia kuwa na chombo imara yaani kuwa na Jukwaa la Uchumi wa Viwanda kama fursa ya kuendelea kuwezesha ujenzi na uendelezaji wa Viwanda Nchini, ambapo wadau watajulishwa tarehe rasmi ya uzinduzi ambao utafanywa na Mh. Waziri Mwijage.


Mkutano huo wa siku tatu kwa njia ya mtandao ulioanza tarehe 18 na kutarajiwa kumalizika 20 Desemba, 2017 umewakutanisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Elisante Ole Gabriel,  Makatibu Tawala wa Mikoa ya Mbeya, Songwe, Kilimnjaro, na Ruvuma, Mikoa mingine ni  Kigoma, Lindi, Singida na Pwani sambamba na wataalamu wao wa Mikoa na wale wa Halmshauri. 

Monday, December 18, 2017

UVUMI WA KINANA KWAMBA HAZIIVI CHUNGU KIMOJA NA JPM MAJIBU YAKE HAYA HAPA.



Ukimya wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Abraham Kinana kufuatia yale yaliyokuwa yakisemwa juu yake umesababisha wengi wadau na wafuatiliaji wa Siasa kuamini kile walichokuwa wakisikia...Mingong'ono imekuwa si kwa wananchi wa kawaida tu au wapinzani wa chama hicho bali pia hata wanachama wa CCM baadhi yao wamesikika mara kadhaa wakinong'ona chini chini kwamba Kinana na JPM haziivi na kabla ya mkutano wa Uchaguzi hii leo 'eTi' alikuwa na mpango wa kukaa kando. 

Kwa takribani siku 3 kabla ya kusanyiko la leo HABARI KUU ILIYOTIKISA IMEKUWA INSHU HIYO.

Nisikuchoshe 

'MAJIBU HAYA HAPA'

MKUTANO MKUU WA CCM WARINDIMA DODOMA, LEO DK. MAGUFULI AMTAKA TENA KINANA, WAJUMBEA WASHANGILIA KUUNGA MKONO

 Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli akifungua Mkutano Mkuu wa tisa wa CCM, katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, Dodoma, leo. Pamoja na mambo mengine kuhusu mageuzi ndani ya Chama, uadilifu na usimamizi wa mali za Chama ili Chama kisitegemee wafadhili wakiwemo matajiri wachache, amemtaka Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana kuendelea kumsaidia katika nafasi hiyo ya Katibu Mkuu katika kipindi kingine cha miaka mitano
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimsalimia Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, alipokuwa akisalimia mabalozi kutoka nchi mbalimbali ambao wamehudhuria Mkutano huo 
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo wakikagua mazingira ya nje ya ukumbi kabla ya mkutano huo mkuu kuanza
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akiandaa mazingira ya kuchangamsha ukumbi kabla ya mkutano huo kuanza. Kushoto ni katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga
 Wanakwaya wa TOT wakiimba wimbo maalum wa kumkaribisha ukumbini Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk John Magufuli
 Wajumbe wakijimwayamwaya ukumbini kushangilia wakati Mwenyekiti wa CCM Taifa, akiingia ukumbini
 Mwimbaji wa TOT akiimba wimbo wa kuhamasisha mapokezi ya Mwenyekiti ukumbini
 Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Jakaya Kikwete na Mwenyekiti mstaafu wa CCM Ali Hassan Mwinyi wakimsubiri Mwenyekiti Kuingia Ukumbini. Mzee Mwinyi akisoma toleo maalum la gazeti la Uhuru wakati akisubiri
 Viongozi waliotangulia meza kuu wakisimama kumlaki Mwenyekiti wa CCM rais Dk John Magufuli wakati akiingia ukumbini
 Mwenyekiti wa CCM Rais Dk John Magufuli akisalimia viongozi mbalimbali baada ya kuingia ukumbini. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
 Mwenyekiti wa CCM Rais Dk John Magufuli akiwa tayari ukumbini. Wengine kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mstaafu Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu Mwenyekiti wa CCM Rais wa Zanzibar Dk. Shein, Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti wa CCM-bara Philip Mangula na Mwenyekiti Mstaaafu wa CCM Benjamin Mkapa
 Mwenyekiti wa CCM Rais Dk John Maguduli akijadili jambo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana baada ya kuketi ukumbini
 Waimbaji wa TOT wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya Mkutano kuanza
 Wajumbe wakiwa wamesimama kuimba wimo wa Taifa
 Mwenyekiti wa CCM Rais Dk John Magufuli na viongozi wengine meza kuu wakiimba wimbo wa Taifa huku wamesimama kwa ukakamavu 
 Viongozi wakiw wameketi baada ya kuimba wimbo wa taifa
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiondoka meza kuu kwa ukakamavu kwenda kufuatilia jambo
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mwenyekiti kufungua Mkutano huo
 Wapicha picha wakifuatilia matukio
 Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere Mama Maria Nyerere akiwa na Mama Salma Kikwete kwenye mkutano huo
 Baadhi ya wageni waalikwa na wajumbea wakiwa kwenye mkutano huo
 Mwenyekiti wa CCM Rais Dk Magufuli (kulia)akifungua mkutano huo mkuu
 Wajumbe wakishangilia baada ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dk Magufuli kumtaka Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kuendelea kumsaidia katika nafasi hiyo ya Ukatibu Mkuu kwa miaka mingine mitano
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akionekana kutafakari baada ya kauli ya Mwenyekiti wa CCM Dk Magufuli  kumhitaji tena
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiinuka kuonyesha ishara ya kukubali makakwa ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. Magufuli. Kulia ni Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Zanzibar Dk Amani Abeid Karume na Mzee Mkapa ambaye anacheka kuonyesha kuunga mkono
 Baadhi ya waliohamia CCM kutoka vyama vya upinzani wakisimama baada ya kutmbulishwa na Mwenyekiti wa CCM Rais Dk Magufuli kwenye mkutano huo
 Mwenyekiti wa CCM Rais Dk Magufuli akipongezwa na Mwenyekiti mstaafu wa CCM Jakaya Kikwete baada ya hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Bara Pius Msekwa 
 "Hotuba imeshiba" inaelekea ndivyo Kikwete alivyomwambia Dk Magufuli baada ya kumpongeza 
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimpongeza Mwenyekiti wa CCM Dk Magufuli baada ya hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo
 Dk Magufuli akipongezwa na Makamu Mweenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula kwa hotuba nzuri ya ufunguzi wa mkutano huo
 Dk. Magufuli akipongezwa na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Zanzibar Amani Karume baada ya hotuba
 Mwenyekiti wa CCM Dk Magufuli akirudi katika nafasi yake baada ya kutoa hotuba na kufungua mkutano huo
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akitoa maelezo kuhusu CCM ilivyotekeleza kazi zake katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. kabla ya hapo alitumia fursa hiyo kumshukuru Mwenyekiti wa CCM Dk Magufuli kwa kumwamini tena ili aendelee kumsaidia. Kinana amemwahidi kumsaidia kwa weledi na uaminifu mkubwa
TOT wakimshangilia Mwenyekiti Dk. Magufuli baada ya hotuba yake

KABLA YA MKUTANO
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM Rais wa zanzibar Dk Ali Mohammed Shein alipowasili kwenye mkutano huo
 Dk Shein akimsalimia Mzee Mkapa
 Dk Shein akimsalimia Mzee Karume. Katikati ni Kikwete
 Dk Magufuli akiongozana na Dk Shein, Mzee Mangula na Ndugu Kinana kwenda ukumbini
 Kabla ya mkutano kuanza, baadhi ya wajumbe wakiperuzi nakala za toleo maalum la gazeti la Uhuru kuhusu mkutano huo
 Wajumbe wakipozi picha ya kumbukumbi ukumbini
 Baadhi ya wafanyakazi waandamizi wa Uhuru Publications Ltd, wachapichaji wa Magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani wakiwa ukumbini
 Mwanadiplomasia akisoma gazeti la Uhuru
 Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM Bara John Chiligati akisoma toleo maalum la gazeti la Uhuru
 Katibu Mwenezi wa CCM Humphrey Polepole akijadili jambo na Afisa Mwandamizi wa CCM Frank Uhahula. kulia ni Kanali Mstaafu Ngemela
 Maofisa wa CCM wakiwa ukumbini kusimamia masuala ya Itifaki
 Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Yusuf Makamba akisalimiana na Mzee John Butiku
 Vijana Jazz wakirindima ukumbini
 Baadhi ya watangazaji wa UHURU FM wakiwa nje ya ukumbi kurusha live matangazo ya mkutano huo mkuu
 Baadhi ya wageni waalikwa wakisalimiana ukumbini
 Mama Janet Magufuli akiwasili ukumbini



 Wajumbe ukumbini

 Wajumbe ukumbini
 Wapigapicha Muhidin Issa Michuzi aka Ankal na Adam Mzee wakicheki mazingira ukumbini
 Wafanyakazi wa Makao Makuu ya CCM, Lumumba wakiwa ukumbini
 Wasanii wa TOT wakipumzika ukumbini baada ya awamu ya kwanza ya kutumbuiza kumalizika. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO