ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 6, 2017

MKUU WA MKOA WA MWANZA AGUSWA NA MAMA HUYU MLEMAVU ALIYEKUWA AKITENGENEZA KIPATO CHAKE KUPITIA BIASHARA YA KUUZA MAJI.

NA ZEPHANIA MANDIA WA G.SENGOBLOG TV



Safari hii ya mkuu wa mkoa wa Mwanza JOHN MONGELA na baadhi ya watendaji wa Mamlaka ya maji safi  na usafi wa mazingira (MWAWASA)  katika mtaa MHANGO C  kata ya nyakato manispaa ya Ilemela kulipia bili ya maji ya VERONIKA MTIRO ambaye ni mlemavu baada ya kushindwa kulipa kwa miezi mitatu.


MONGELA anasema mama huyo alikuwa anajikimu kupitia maji hiyo hivyo ameamua kumlipia baada ya mama huyo kuomba msaada wa ofisi yake.

Veronica anasema changamoto hiyo imejitokeza baada ya kuumwa kwa muda wa miezi mitatu hivyo kushindwa kulipa bili ya maji laki moja na 39 kwa miezi mitatu ,na  aliyokuwa anauza maji kama njia ya kujipatia kipato sambamba na ufundi wa kuchomelea vyuma amabayo pia hana uwezo wa kununua vitendea kazi.



MWENYEKITI MPYA CCM, KAMATI YA SIASA YACHAGULIWA KWA KISHINDO WILAYA YA SINGIDA VIJIJINI

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Singida Vijijini Bi Grace Shindika akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini.
Kamati ya Siasa Wilaya ya Singida Vijijini ikijihuzuru mbele ya wajumbe muda mchache kabla ya mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Singida Vijijini akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Singida Vijijini akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini.
Msimamizi wa uchaguzi akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini.
Wajumbe wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini wakifatilia kwa makini mkutano wa uchaguzi.
Wajumbe wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini wakifatilia kwa makini mkutano wa uchaguzi.

Na Mathias canal, Singida

Wajumbe wa Mkutano mkuu maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida  Vijijini Mkoani Singida wametumia haki yao ya kidemokrasia kwa kufanya uchaguzi wa kuwapata viongozi wa ngazi mbalimbali za Wilaya, wawakilishi wa ngazi ya mkoa na Taifa.

Mkutano huo ulifanyika katika Kijiji na Kata ya Ilongelo na kuhudhuruwa na wajumbe waliozidi akidi ya matakwa ya mkutano wa CCM Wilaya kwa mujibu wa maelekezo ya kanuni za uchaguzi wa CCM.

Mwenyekiti mpya wa CCM Wilaya ya Manyoni aliyechaguliwa kwa kura za kishindo ni William Mwang'ima Nyalandu aliyepata kura 440, akifatiwa na FATUMA Ihonde aliyepata kura 189 na nafasi ya tatu ilikamatwa na Alex Mdidi Lissu aliyepata kura 159.

Akizungumza na Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Singida Vijijini Bi Grace Shindika alisema kuwa uchaguzi huo umekamilika kwa amani na salama kwa kufuata taratibu na kanuni za uchaguzi zilizoelekezwa na Chama Cha Mapinduzi.

Alisema kuwa pamoja na nafasi hiyo ya mwenyekiti wa CCM Wilaya lakini pia nafasi zingine zilizowaniwa ilikuwa ni pamoja na Nafasi Ya Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya  ambapo Richard Niangusha Kwimba aliibuka mshindi kwa kupata kura  6, nafasi ya pili ni Khamisi Swalehe Kimu kura 35, Iddi Athumani Monko kura 8 na Swalehe Munkumbu Sungi aliyepata kura 3.

Nyingini ni nafasi ya mkutano Mkuu wa CCM Taifa waliomba ridhaa katika nafasi hiyo ni watu 14 ambapo kati yao washindi ni Sabasaba Manase, Zainabu Abdaleah na Khadija Kisuda Lesso.

Nafasi ya Halmashauri Kuu ya Wilaya waliogombea ni 27 ambapo kati yao walioshinda ni Sabasaba Manase, Edward Jared Ihondo, Japhet Ntandu Gham, Justin Joseph Monko, Mohamed Abdallah Ghamayu, Nkumbi Mohamed Kemi, Zuena Dunya, Simon Mumbai, Shabani Ally Mang'ola, na Wiliamu Mwang'imba Nyaland.

Nafasi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa waliomba  walikuwa watano lakini washindi kati yao ni Mchungaji Wilson Mtatuu Ihucha, na  Sada Njiku. Wajumbe wa Kamati ya siasa Mkoa ni Sabasaba Manase, Shaban Mang'old na Edward Jared Ihonde.

Katibu huyo wa CCM Mkoa wa Singida Bi Grace Shindika alisema kuwa huu ni wakati wa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa kati ya wananchama na viongozi wote waliochaguliwa ili kuongeza ufanisi na nguvu ya chama katika Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla.

WASTAAFU WAIPONGEZA PSPF KWA KUPOKEA MALIPO YA PENSHENI YA MWEZI KWA WAKATI


 Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Mwanjaa Sembe, (wapili kushoto), akimkabidhi kijarida cha Mfuko huo chenye maelezo ya shunguli mbalimbali zinazotekelezwa na PSPF, kwa Mwanachama wa Mfuko amabye ni Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mstaafu, Mzee Thomas Martin  Kiama, (73), nyumabni kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja leo Oktoba 6, 2017. Wengine pichani kutoka kushoto, ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, na Afisa wa Unedeshaji Bw. Ernest Massay.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WANACHAMA wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, ambao ni wastaafu, wameupongeza Mfuko huo kwa kupata pensheni za kila mwezi kwa wakati.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya viongozi wa PSPF kutembelea Wanachama wake wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma Kwa Wateja Duniani, walisema kimsingi malipo ya pensheni ya kila mwezi yamekuwa yakiingia kwenye akaunti zao kwa wakati na bila usumbufu wowote.
“Mimi nashukuru penshni yangu napata bila shida, na inaingia kwenye akaunti yangu kwa wakati, hili napenda kuwapongeza sana.” Alisema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Mstaafu). Bw. Thomas Martin Kiama wakati alipotembelewa na ujumbe wa PSPF nyumbani kwake Oysterbay jana (Oktoba 6, 2017).
Najua zipo changamoto za hapa na pale, mimi ningependa muwe huru kabisa, ili muweze kutuhudumia vema sisi wanachama, vinginevyo huduma zenu nazifurahia, aliongeza Bw.Kiama, ambaye alistaafu mwaka 2005.
Kwa upende wake, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, nchini, Bibi. Mary Hariet Longway, naye aliipongeza PSPF kwa utoaji wa huduma na kwamba yeye anaridhishwa na utedaji kazi wake na kuwapongeza kwa kufika nyumbani kwake ili kupata maoni yake.
“Ninashukuru sana kwa kunitembelea kwani hii ni ishara ya jinsi mnavyotujali sisi wastaafu, lakini mimi kama Jaji mstaafu kwa utaratibu ulivyokuwa, sisi hatukuwa na bima za afya sasa kama mngetoa elimu ya jinsi ya kupata bima ya afya kupitia kwenu lingekuwa jambo jema.” Alishauri Bibi Longway amabye naye alistaafu mwaka 2005.
Alsiema, malipo ya kila mwezi ya Pensheni yake yamekuwa yakiingia kwenye akaunti yake bila shida yoyote.
Naye askari wa Jeshi la Magereza (mstaafu), Bw.Kasim Salehe Mafanya, yeye naye aliipongeza PSPF, kwa huduma bora lakini akaomba utaratibu ufanyike ili pensheni hiyo iweze kuboreshwa na hivyo kuelndelea kuwa na manufaa zaidi.
Akizungumza kwa niaba ya PSPF, Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, Bi. Mwanjaa Sembe, alisema, katika kuadhimisha Wiki ya Wateja Duniani, ofisi za PSPF kote nchini, zimefanya utaratibu wa kuwatembelea wanachama wake kwa lengo la kuwahakiki na kupokea maoni yao ili kuboresha utoaji wa huduma.
Aidha katika Ofisi za Makao Makuu, Wakurugenzi an Mameneja waliungana na maafusa na wafanyakazi wa Mfuko huo, katka kuwahudumia wateja waliofika makao makuu.

 Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa nchini, Bibi Mary Logway, ambaye  ni mwanachama wa PSPF, akizungumza nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam leo Oktoba 6, 2017, wakati alipotembelewa na Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa PSPF, Bi. Mwanjaa Sembe, kushoto.
 Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, (wakwanza kushoto), akimsikilzia mteja (mwanachama) wa Mfuko, huku afisa aliye kwenye mafunzo kutoka Chuo Cha Usimamzi wa Fedha, (IFM), Bw. Paschal W. Divaz, (katikati), akifuatilia.
 Bw. Silayo akisalimiana na wateja (wanachama) waliofika makao makuu ya Mfuko kuhudumiwa.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa PSPF, Bi. Neema Muro, (kulia), akimuhudumia mteja (mwanachama) aliyekifa makao Makuu kuhudumiwa.
Meneja wa Huduma kwa Wateja, PSPF, Bi. Laila Maghimbi, (kulia), na mteja wake, (mwanachama) wakifurahia jambo wakati mwanachama huyo akipatiwa huduma.
  Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, wapili kulia), akizungumza na afisa aliye mafunzoni, kutoka chuo cha Usimamizi wa Fedha, 9IFM), Bw.Paschal W. Diaz
 Afisa Uchangiaji wa Hiari PSS, Bi.Mwajuma A.Mohammed, (kushoto), akimuhudumia mteja.
Afsia Mtekelezo, (CO), wa PSPF, Bi. Mwanaisha S. Waziri akiwa kazini.
 Afisa wa PSPF aliye mafunzoni, Bw. Alpha Mkopi, (katikati), akiwahudumia wateja, waliofika ofisi za Makao Makuu kupata huduma.
Maafisa wa PSPF wakitoa huduma Oktoba 6, 2017.
Mzee Kiama, (kushoto), akipitia maelezo ya uhakiki kabla ya kuweka saini yake. aliye nae ni Meneja wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), Bi. Mwanjaa Sembe.
 Mzee Kiama akiweka saini kwenye fomu ya uhakiki.
Bi. Mwanjaa Sembe, (kushoto), akimpa maelezo, Jaji Mstaafu, Bi. Mary Longway, kuhusu uhakiki wa uanachama wake PSPF.
Bi. Longway akiweka saini wkenye fomu hiyo ya uhakiki.
 Mkuu wa kitengo cha Mikopo kwa Wanachama wa PSPF, Bi. Linda Bahati, akizungumza na simu ya kikazi ili kupata maeelzo ya ziada wakati akimuhudumia mteja Oktoba 6, 2017.
 Afisa Uhsuiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi akizungumza na Mzee Kiama.
Jaji (mstaafu) Longway na mukuu wake, wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyaakzi wa PSPF waliomtembelea ofisini kwake Upanga jijini Dar es Salaam Oktoba 6, 2017.

DC MTATURU AKUTANA NA WATAALAMU WA KILIMO IKUNGI KUJADILI UBORESHAJI SEKTA YA KILIMO.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo wakati wa kikao Cha kazi na wataalamu wa Kilimo, Mifugo, Ardhi, Maliasili na mazingira.

Wataalamu wa kilimo, Mifugo, Ardhi, Maliasili na mazingira wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa kikao cha kazi.
Afisa Kilimo na Mifugo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ayoub Sengo (aliyesimama) akizungumza jambo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu, Mwingine ni Afisa Tawala Wilaya ya Ikungi Dandala Mzunguor.

Wataalamu wa kilimo, Mifugo, Ardhi, Maliasili na mazingira wakishauri jambo wakati wa kikao kazi na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu.


Na Mathias Canal, Singida

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu amekutana na kufanya kikao cha kazi na wataalamu wa Kilimo, Mifugo, Ardhi, Maliasili na mazingira kubaini kwa pamoja mbinu bora za kuwasaidia wakulima kuzalisha mazao ya chakula na biashara kwa wingi.

Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na Maafisa kilimo na Mifugo, Maafisa Ardhi, Maliasili na Mazingira, Maafisa Ugavi wa Kata sambamba na Maafisa Tarafa, Mtaturu amesema kuwa bado uzalishaji wa mazao ni mdogo katika Wilaya ya Ikungi ukilinganisha na hali ya hewa ikiwa ni pamoja na kuwa na ardhi nzuri.

Amewataka wataalamu hao wa kilimo kuwasaidia wakulima ili kuiwezesha Sekta ya Kilimo, kutoka kilimo cha kujikimu kuwa kilimo cha kibiashara, kitakachowezesha kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na kupunguza umasikini kwa watanzania Sambamba na kujitosheleza kwa chakula.

Mtaturu amesema ili kilimo kiwe kizuri na chenye tija kwa wananchi, Wataalamu wanapaswa kuzingatia uwepo wa pembejeo na mbegu bora za kisasa na kuhuisha kilimo cha umwagiliaji kwa kuandaa mpango wa kujenga skimu za umwagiliaji.

Ameongeza kuwa serikali imetoa tani 20 za mbegu za kamba katika Wilaya ya Ikungi ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo ambapo zitagawanywa kwa wakulima ili msimu wa kilimo unapoanza tayari kusiwe na kucheleweshwa kwa mbegu hizo.
Pia amewaagiza maafisa ugani kuwa na mashamba darasa kwani kupitia wao yatawasaidia wakulima kuwa na uelewa mkubwa katika kuongeza ufanisi wa kilimo chenye tija.

Aidha, amesema Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania imeanzisha huduma zake kanda ya Kati Dodoma ambapo mikopo ya aina mbalimbali hutolewa kuwezesha wakulima kuongeza tija na uzalishaji katika sekta ya kilimo nchini Tanzania.

Mtaturu amesema ni vyema kama wataalamu wa kilimo watatumia nafasi hiyo kuwaunganisha wakulima na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa Masoko na kuongeza Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo.

Katika kikao hicho cha kuwakumbusha majukumu wataalamu hao Mtaturu amewataka kuandaa mpango kazi wa mazao ya kilimo hususani mazao ya chakula na biashara.

Mtaturu amewaelekeza wataalamu hao wa kilimo kuwasisitiza wananchi katika maeneo yao kuanza kulima mazao ya kipaumbele yaliyoelekezwa na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa ambayo ni zao la Pamba, Korosho, Chai, Kahawa na Tumbaku.

Amesema pomoja na mazao hayo ya kipaumbele lakini pia wananchi wanapaswa kuendelea kuongeza nguvu katika mazao yanayostawi kwa wingi Wilayani humo ikiwa ni pamoja na zao la alizeti, mtama, mahindi na zao la dengu.

Katika upande mwingine Mtaturu ameshauri wataalamu wa Mifugo kutilia msisitizo Ufugaji wa kisasa (Ziro Grazing) kwa kutembelea na kupata utaalamu wa Ufugaji na mbegu Bora za ya Ng'ombe wa kisasa kwa wataalamu katika Rachi ya Taifa ya Kongwa (NARCO) na LITI iliyopo Mpwapwa Mkoani Dodoma.
Sambamba na hayo pia Mkuu huyo wa Wilaya ameagiza heka 1500 ambazo ni kichaka kuandaliwa utaratibu kwa ajili ya kilimo ili kuongeza uzalishaji wa kilimo.

Naye Afisa Kilimo na Mifugo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Ayoub Sengo amepongeza kasi ya uwajibikaji ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu kwa ufanisi wake kusaidia kuonyesha njia jambo ambalo linapelekea kubadili fikra za wakulima na wananchi kwa ujumla.

Sengo amempongeza Mkuu huyo wa Wilaya ya Ikungi kwa kuwezesha kupatikana muwekezaji ambaye atakayepewa heka 1000 na serikali ya kijiji kwa ajili ya kilimo cha korosho zao ambalo litakuwa na tija kwa pande zote mbili kwani pia wananchi watanufaika na huduma za ugani.

WAKULIMA WA PAMBA WILAYANI GEITA WAIOMBA SERIKALI KUTATUA KERO YA PEMBEJEO NA WATAALAM WA KILIMO.

Shamba la Pamba.
Afisa Kilimo  wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Samweli Abuye  akizungumza na wakulima wa Kijiji na Kata ya Kagu.

Baadhi ya wananchi wakifuatilia kwa umakini maelekezo ya Kilimo cha pamba ambacho kinatarajia kuanza hivi karibuni.

Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akizungumza na watendaji wa kata na vijiji na kutoa msisitizo wa kuwasisitiza wananchi kwenye maeneo yao kulima zao la Pamba.







PICHA NA JOEL MADUKA 





Wakulima  wa zao la pamba katika tarafa ya Bugando Wilaya na Mkoani  ya Geita wamesema  wamekuwa wakikata tamaa kuendelea na kilimo cha zao hilo kutokana na sababu mbalimbali wanazokumbana nazo likiwemo suala la pembejeo pamoja na bei za pamba kutokueleweka.

Wakizungumza katika kikao cha maelekezo kwa watendaji wa serikali ya Vijiji na Kata kwenye ukanda wa tarafa ya Bugando, wakulima wa zao hilo  Faustin Nyamhanga, Faida Mwendesha  na Mateso Kabegelo, wameyatupia lawama makapuni yanayojihusisha na ununuzi wa zao hilo  kwa kile walichodai kwamba wanakuja na bei yao mkononi ambayo ni ya ughalalizaji.

Pamoja na mambo mengine, wameendelea  kuikumbusha serikali kuendelea kuyapatia ufumbuzi masuala ambayo yameonekana kuwa ni changamoto kwa wakulima.

Diwani wa kata ya Nyamboge, Daudi Bakazahala ameiomba Idara ya Kilimo Wilayani humo  kushirikiana na  Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoa wa Geita ili kushughulika na wahasibu wa makampuni ya ununuzi wa pamba kwenye maeneo ya vijijini ambao wamekuwa na tabia ya kuwaibia wakulima.

Kutokana na kero ambazo zimeelezwa na wakulima pamoja Diwani, Mkaguzi wa Zao la pamba Wilaya ya Geita Venance Kankutebe, amesema kutokana na uchache wa viwanda imekuwa ni changamoto kwa upande wa bei, huku Afisa Kilimo Samweli Abuye akijibu ombi la diwani wa Nyamboge kwa kubainisha kwamba ni vyema wao kama viongozi wa kata kumfikishia mwenyekiti ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Geita Juu ya madai ambayo wamekuwa nayo kwani yeye ndiye msimamizi mkuu wa kikosi kazi cha ufuatiliaji wa kilimo cha pamba.