ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 17, 2017

PAPA FRANCIS: TAMAA YA MADOLA MAKUBWA IMESABABISHA UMWAGAJI DAMU DUNIANI.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani ametahadharisha kuhusiana na hatua za kupenda vita za madola makubwa duniani na kusema kuwa, tamaa ya madola hayo imesababisha umwagaji duniani.
Papa Francis amesema kuwa, madola makubwa yakiwa na lengo la kunufaika na kushika hatamu za uongozi yamekuwa sababu ya kutokea vita na umwagaji damu katika maeneo mbalimbali ulimwenguni.
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani amesema bayana kwamba, yanachokitafuta madola makubwa duniani ni nguvu, satwa na kunufaika. Papa Francis ameeleza kuwa, siasa za kupenda vita zimekuwa ni tishio kubwa mno kwa maisha na utulivu wa walimwengu.
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani ametoa wito wa kudumishwa amani na kuchukuliwa hatua za kukomesha vita na machafuko katika maeneo mbalimbali ulimwenguni.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani anabainisha hayo katika hali ambayo, maelfu ya watu wamepoteza maisha yao katika miaka ya hivi karibuni ikiwa ni natija ya uingiliaji wa kijeshi wa Marekani na waitifaki wake wa Kimagharibi katika nchi za Iraq, Syria na Yemen.
Aidha asasi za kimataifa kama Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama la Umoja huo zinakosolewa mno na walimwenghu kutokana na kuathiriwa katika utendaji wake na madola makubwa.
Udhaifu wa taasisi hizo umezifanya zshindwe kutekeleza majukumu yao ipasavyo na hivyo kubakia kama wenzo unaotumiwa na madola makubwa kwa ajili ya kufikia malengo yao.

POLISI MWANZA YAKAMATA BHANGI NA DAWA ZA KULEVYA.

NA ANNASTAZIA MAGINGA,Mwanza

WAKATI sakata la dawa za kulevya likipamba moto nchini Jeshi la polisi mkoani hapa linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kukutwa na misokoto 59 ya bangi pamoja na madawa yanayodhaniwa kuwa ni ya kulevya yaitwayo kabasanda kiasi cha kilo moja.

Tukio hilo limetokea  February 14 mwaka huu saa 11 jioni maeneo ya Nyakato kata ya Nyakato Wilaya ya Nyamagana Mkoani hapa ambapo askari wakiwa kwenye doria na misako walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema juu ya uwepo wa watu hao.

Akiwataja watuhumiwa hao mbele ya waandishi wa habari jana Naibu kamishina wa polisi Ahmed Msangi alisema kuwa ni Vitarius Mtasingwa (35) , Bhoke  Sam (36), Alladini Hussein (44) wote wakazi wa Nyakato National

Ameeleza kuwa awali askari wakiwa kwenye misako na doria walipokea taarifa kutoka kwa raia kuwa kuna watu wanaosadikika kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya na kwamba askari walifanya ufuatiliaji wa haraka maeneo hayo na kufanikiwa kuwakamata wote watatu.

Aidha amesema  kuwa  baada ya tukio hilo askari waliendelea na doria katika maeneo tofauti ambapo ilipofika saa 01.30usiku  February 15,mwaka huu maeneo ya hotel Mwanza  Wilaya ya Nyamagana , askari walifanikiwa kumkamata mtummoja aliyejulikana kwa jina la Mwalimu Mohamed (30), mkazi wa Kirumba akiwa na noti 46 za sh Elfu kumi  zenye jumla ya thamani ya  sh 460,000kitendo ambacho ni kosa la jinai.

“Wakati huo askari wetu wakiwa doria katika maeneo hayo walipata taarifa ya kutoka kwa raia wema kwamba yupo mtu ambaye walimtilia shaka kwamba ni mhalifu  ndipo askari wafika kwenye eneo hilo na kuweza kumkamata”alisema Msangi.

Aidha polisi wanaendelea na mahojiano  na watuhumiwa wote wanne, na kwamba taratibu zinafanya zinafanyika za kupeleka mimea ya kabasanda iliyokamatwa kwa mkemia wa serikali ili kuweza kubaini kama ni madawa ya kulevya  au laa , pindi uchunguzi utakapo kamilika watafikishwa mahakamani na kwamba  misako  ya kuwatafuta  watu wengine  ambao wanadaiwa kushirikiana na watuhumiwa tajwa.

WAZEE HALMASHAURI YA WILAYA YA SENGEREMA WAKUMBUKWA

Halmashauri ya wilaya ya Sengererma imezindua vitambulisho kwa wazee ili kupata matibabu bure

Akizungumza na wazee hao  katika kata ya IGALULA wilayani humo  mkuu wa wilaya ya Sengerema mh Emanuel Kipole amewataka wananchi kufanya kazi ilikuleta maeendeleo ya taifa kwa kuwa serikali ya awamu ya tano inawataka watu wafanye kazi.

cue in MH KIPOLE 01 KAZI

Mh kipole amewapongeza wazee hao  na  kusema kuwa serikali inatambua mchango wa wazee na busara pia katika kulitumikia taifa na hata kupigania uhuru hivyo itaendelea kuwaenzi wazee  hasa upande wa afya kwakuwa mtaji mkubwa wa maisha ya mwanadamu ni afya.e
  
Akizungumzia mpango wa serikali kwa wazee  mh.Kipole amsema kuwa wazee wote kuanzia umri wa miaka 60 serikali itahakikisha wanapata huduma za afya bure bila malipo ,na zoezi hili la vitambulisho  limeanza mwaka jana na tayari wazee 2001 wamekisha kupatiwa  vitambulisho na bado linandelea.

Akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa wilaya ya Sengerema  Magesa Mafuru  Bonifasi amesemakuwa zoezi hili nimefanyika kwa ufanisi, na kufanikiwa kuwahamasisha  wazee 651 na wazee 51 watakabidhiwa vitamburisho kwa kuwawakilisha wazee wengine katika kata nyingine na kuongeza kuwa katika zoezi hili mabalaza mbali mbali yameundwa kuanzia kijiji ,kata na mbalaza la wazee la wilaya.

Naye mganga mkuu  wilaya Sengerema Dr .Petel Mangu amesema kuwa kazi hii ni kutekeleza maelekezo ya serikali kwa kuanzisha baraza na kutengeneza kumbukumbu za wazee katika wilaya na kuwapatia vitamburisho kwa huduma za matibabu na tayari wamefanikiwa kuunda baraza la wazee kwa ngazi ya  kijiji na kata wakichuchumilia ngazi ya wilaya. 

Idara ya afya Halmashauri ya Sengerema imepanga kutengeneza vitamburisho 651 kwa miezi 6, na kwamiezi zita ijayo vitatengenezwa vitamburisho 651 na vitamburisho vilivyotengenewa ni kwa kata 13 kati ya kata 26.

Nao wazee wametoa maoni yao kwa kuipongeza serikali kwa kuwaajali wazee changamoto ni upatikanji wa dawa katika hospitali 

Thursday, February 16, 2017

MKURUGEZI WA MWAUWASA ASAINI MIKATABA YA ZAIDI BILIONI 240

ZEPHANIA MANDIA,MWANZA
 WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge amewataka Wakandarasi wa Miradi ya Maji  Safi na Usafi wa Mazingira kwa Jiji la Mwanza kuzingatia ubora katika kazi zao pamoja na kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa muda uliyopangwa.

Waziri Lwenge alisema hayo mkoani hapa wakati akisaini mikataba ya Ujenzi wa miradi hiyo, serikali kwa kushirikina na wadau wa maendeleo wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) pamoja na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD).

“Miradi hii itajumuisha miji sita ambayo ni Mwanza, Musoma, Bukoba, Misungwi na Lamadi. Ninachotaka ni kwamba ikamilike kwa wakati na kazi ifanyike kwa viwango na ubora unaohitajika. Mtambue kuwa kiasi cha sh.bilionin 245 zitatumika kwenye  mradi huu,fedha hzio ni nyingi naomba kazi hiyo ifanyike kwa ufasaha,”alisema Mhandisi Lwenge.pia alimpongeza mkurugenzi wa mwuwasa injinia Anthon Sanga,kwakusimamia miradi mikubwa ya serikali.

Alisema Benki ya Maendeleo ya Ulaya pamoja na Shirika la Maendeleo la Ufaransa wanachangia sh. bilioni 105 kila mmoja ikiwa ni mkopo wenye masharti nafuu, ambapo Serikali ya Tanzania imechangia sh. bilioni 34 ambayo ni sawa na asilimia 14.

“Fedha hizi zinakusudiwa kunufaisha Jiji la Mwanza kwa kiasi cha sh.bilioni 133.7, Miji ya Bukoba na Musoma kwa kiasi cha sh.bilioni 62.5 na Miji ya Lamadi, Magu na Misungwi kiasi cha sh.bilioni 37.6, sh. bilioni 11.2 sawa na asilimia 5 zitakuwa ni gharama zitakazotumika katika usimamizi wa mradi,”alisema  Mhandisi Lwenge.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mkoani Mwanza (Mwauwasa), Antony Sanga.

Akizungumza baada ya kuwekeana saini hizo, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mkoani Mwanza (Mwauwasa), Antony Sanga alisema: “Mradi huu utanufaisha idadi kubwa ya wakazi wa Mwanza. Tunaimani wale waliyokuwa wakikosa maji watapata vizuri. Maneo ya milimani nayo tunatarajiwa kuwa yatapata maji ya uhakika tofauti na ilivyokuwa awali.”
Lwenge alisema katika Jiji la Mwanza wakazi 105,649 wanaoishi katika maeneo ya miinuko watanufaika, wakazi wa Lamadi watakaonufaika ni 23,540, Magu 45,340 na Misungwi 23,315 na kwamba mradi huo utakamilika katika kipindi cha mizei 18.

“Kukamilika kwa miradi hii kutaongeza upatikanaji wa maji katika Jiji la Mwanza kutoka wastani wa asilimia 90 kwa eneo la mijini kwa sasa hadi kufikia asilimia 96 ifikapo 2019,”alisema.

ELIMU IMEIPA MWANZA UJASIRI KUPIMA HIV BILA KUSUKUMWA.

Na James Timber,
GSENGO BLOG Mwanza
WATU
zaidi ya 400, mkoani Mwanza, wamejitokeza kupima virusi vya ukimwi sambamba njia ya uzazi wa mpango.

Hayo yalisemwa na  Mratibu wa Vijana wa Shirika la Marie Stopes Tanzania Daniel Mjema mara baada ya zoezi la  kuhudumia wananchi   la kupima afya kwa hiari, iliyotolewa na shirika hilo mtaa wa National kata ya Nyakato wilayani Ilemela mkoani hapa.

Mjema alisema kwa sasa muitikio wa watu ni  mkubwa ,kwani katika zoezi hilo lililofanyika kwa siku 3, watu  487 walijitokeza, huku wa uzazi wa mpango  261 na VVU 226.

Alisema, licha ya mwitikio kuwa mkubwa,watu wanatakiwa kujitokeza zaidi linapotokea suala la upimaji,ili waweze kupata huduma,elimu pamoja na kutambua afya zao.

Vijana wengi wamejitokeza katika zoezi la upimaji sambamba na makundi mbalimbali, kwani kupima na kutambua afya ni bora, kuliko kusubilia mpaka kuugua,hivyo jamii inatakiwa kuendelea kujitokeza endapo kunatokea huduma ya upimaji, " alisema Mjema.

Pia alisema, shirika hilo linawafikia  na watu vijijini kupitia huduma yao ya vikoba,licha ya kukutana na changamoto ya mila potofu.

Hata hivyo alisema, wanapita vyuoni, ili kuhamasisha vijana kupima afya zao, sambamba na kuelimisha juu ya afya ya uzazi na utumiaji njia ya uzazi wa mpango.

Aidha alisema, kuna sheria zinazo wabana, ili waweze kuanza kutoa elimu ya afya ya uzazi na VVU, kuanzia shule ya msingi, kwani wao ndio waathirika zaidi katika suala la mimba za utotoni.

Kadhalika alisema, shirika hilo na mashirika mengine,wanaendelea kuishawishi serikali, ili iwapatie kibali kwa ajili ya kutoa huduma hiyo kwa vijana wa shule za msingi.

MANJI AREJEA URAIANI.

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji ameachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni 10. Manji alipandishwa kizimbani leo kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa shtaka la kutumia dawa za kulevya.
Manji amedhaminiwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa. Kabla ya hapo mfanyabiashara huyo alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya Muhimbili kutokana na matatizo ya moyo yaliyompata baada ya kushikiliwa kwenye kituo kikuu cha polisi Central.

ZANTEL, BAKWATA WAZINDUA HUDUMA YA MPYA YA “ZANTEL MADRASA JIJINI DAR ES SALAAM

Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeiry akizungumza mapema leo jijini Dar es salaam katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya kutoka Zantel iliyopewa jina la ‘Zantel Madrasa’ ambayo ni mahususi kwa waumini wa dini ya Kiislamu kujifunza imani ya dini hiyo pamoja na kupata mafundisho kupitia simu za mkononi ambapo kwa watumiaji wa mtandao wa Zantel watakaopenda kutumia huduma hii watatakiwa kupiga simu au kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 15586 na kufuata maelekezo. (katikati) ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin na Mkuu wa kitengo cha huduma na bidhaa Zantel Hamza Zuheri.

Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Benoit Janin.

Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeiry na Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Benoit Janin wakionyesha vipeperushi vya huduma mpya ya ‘Zantel Madrasa’ kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma hiyo uliofanyika mapema leo jijini Dar es salaam

Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeiry akitoa salamu na kugawa vipeperushi kwa baadhi ya wageni waalikwa mapema leo jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Zantel Madrasa’ itakayopatikana kupitia mtandao wa Zantel ikiwa ni mahususikwa waumini wa dini ya Kiislamu kujifunza imani ya dini hiyo pamoja na kupata mafundisho kupitia simu za mkononi.

Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeiry akitoa salamu na kugawa vipeperushi kwa baadhi ya wageni waalikwa mapema leo jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Zantel Madrasa’ itakayopatikana kupitia mtandao wa Zantel mahususi kwa waumini wa dini ya Kiislamu kujifunza imani ya dini hiyo pamoja na kupata mafundisho kupitia simu za mkononi. (Katikati) ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Benoit Janin pamoja na Mkuu wa Kitengo cha huduma na bidhaa Zantel Bw. Hamza Zuheri.

Mwandishi wa gazeti la The Citizen Alawi Masare (Kushoto) akifanya mahojiano na Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Benoit Janin (katikati) na Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano Zantel Rukia Iddi Mtingwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Zantel Madrasa’ ambayo ni mahususi kwa waumini wa dini ya Kiislamu kujifunza imani ya dini hiyo pamoja na kupata mafundisho kupitia simu za mkononi.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
ZANTEL, BAKWATA WAZINDUA HUDUMA YA MPYA YA “ZANTEL MADRASA JIJINI DAR ES SALAAM
·        Waumini  wa dini ya Kiislamu sasa watajifunza masuala ya dini kupitia simu za mkononi
16 Februari 2017, Dar es Salaam- Zantel kwa kushirikiana na Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) imezindua huduma mpya inayojulikana kama ‘Zantel Madrasa’ ambayo itawawezesha waumini wa dini ya Kiislamu kujifunza kuhusu imani ya dini hiyo pamoja na kupata mafundisho kupitia simu zao za mkononi.
Huduma hiyo itajumuisha mambo mbalimbali kama vile Hadithi, Quran, Dua na huduma nyingine nyingi kupitia ‘App’ kwenye simu ya smartphone ((IVR/SMS/Mobile App and Bakwata News), ambapo pia mteja ataweza kupata taarifa kwa kupiga simu.
Akizungumza wakati wa sherehe ya uzinduzi wa huduma hiyo mpya jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin alisema, “Tunafuraha kuzindua huduma hii ya ‘Zantel Madrasa’ ambayo itawaunganisha waumini wa dini ya Kiiislamu nchini na kuwawezesha kupata maarifa ya dini hiyo kwa urahisi zaidi.”
Kwa upande wake Sheikh Mkuu wa BAKWATA, Mufti Abubakar Zuberi ambae alikua mgeni rasmi alisema, “Hii ni huduma ya kipekee kwa jumuiya ya Waislamu na kila mtu anayependa kujifunza kuhusu dini ya Kiislamu. Nawaomba Waislamu wenzangu kutumia fursa hii mpya na mjiunge kwa wingi ili kujua mambo yanayopaswa kufanywa katika Uislamu.”
“Ninaamini kwamba huduma hii mpya itarahisha kazi kwetu viongozi wa Kiislamu kwa kuwa mafundisho mengi yatakuwa yanapatikana kupitia Zantel Madrasa,” alisema.

Aliongeza kwamba BAKWATA itaisaidia Zantel kuitangaza huduma hiyo hapa nchini Tanzania hususan katika misikiti.

Zantel Madrasa ni huduma ya kwanza kuzinduliwa kwenye mitandao ya simu nchini Tanzania ikilenga kutoa mafundisho ya dini na kuwaunganisha watu kujifunza kuhusu dini nchini.
Huduma hii inatoa fursa kwa Waislamu wote kujiunga na huduma hii kwa kupitia namba maalumu za mtandao wa Zantel, hivyo kuwezesha watumiaji wa simu zaidi ya milioni 1 kupata mafunzo ya Madrasa kwa siku.

Watumiaji wa mtandao wa Zantel ambao watapenda kuitumia huduma hii watatakiwa kupiga simu au kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 15586 na kufuata maelekezo utakayopewa ili kuunganishwa na kufurahia huduma hii.

ZANTEL, BAKWATA WAZINDUA HUDUMA YA MPYA YA “ZANTEL MADRASA JIJINI DAR ES SALAAM

Photocaption 2 &2b
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeiry akizungumza mapema leo jijini Dar es salaam katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya kutoka Zantel iliyopewa jina la ‘Zantel Madrasa’ ambayo ni mahususi kwa waumini wa dini ya Kiislamu kujifunza imani ya dini hiyo pamoja na kupata mafundisho kupitia simu za mkononi ambapo kwa watumiaji wa mtandao wa Zantel watakaopenda kutumia huduma hii watatakiwa kupiga simu au kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 15586 na kufuata maelekezo. (katikati) ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin na Mkuu wa kitengo cha huduma na bidhaa Zantel Hamza Zuheri.

Photocaption 6 & 6b
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeiry na Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Benoit Janin wakionyesha vipeperushi vya huduma mpya ya ‘Zantel Madrasa’ kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma hiyo uliofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.

Photocaption 7& 7b
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeiry akitoa salamu na kugawa vipeperushi kwa baadhi ya wageni waalikwa mapema leo jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Zantel Madrasa’ itakayopatikana kupitia mtandao wa Zantel ikiwa ni mahususikwa waumini wa dini ya Kiislamu kujifunza imani ya dini hiyo pamoja na kupata mafundisho kupitia simu za mkononi.

Photocaption 8
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeiry akitoa salamu na kugawa vipeperushi kwa baadhi ya wageni waalikwa mapema leo jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Zantel Madrasa’ itakayopatikana kupitia mtandao wa Zantel mahususi kwa waumini wa dini ya Kiislamu kujifunza imani ya dini hiyo pamoja na kupata mafundisho kupitia simu za mkononi. (Katikati) ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Benoit Janin pamoja na Mkuu wa Kitengo cha huduma na bidhaa Zantel Bw. Hamza Zuheri.

Photocaption 12