ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, December 3, 2017

WAZIRI NISHATI NA MADINI ARIDHISHWA NA MRADI WA UMEME WA REA MISUNGWI.

Waziri wa Nishati Dkt,Medard Kalemani ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi wa usambazaji Umeme na kuipongeza Kampuni ya Nipo Group Co.Ltd ya Dodoma kwa  kutekeleza mradi huo km.8 katika Vijiji vya Kata ya Mondo na Mwaniko Wilayani Misungwi.
Waziri Kalemani amezungumza na kuwaeleza haya Wananchi wa Kata ya Mwaniko wakati akiwahutubia Mara baada ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa mradi wa kusambaza miundombinu ya umeme katika Mkoa wa Mwanza Wilayani Misungwi kupitia REA awamu ya tatu iliyoanza mapema mwenzi Juni mwaka 2017 na Vijiji 22 vya Wilaya ya Misungwi vitanufaika na mradi huo.

Dkt,Kalemani amempongeza Mkandarasi wa Kampuni ya Nipo Group Co.Ltd kwa kazi anayoifanya ya kusambaza Umeme vijijini kwa haraka na kumtaka kukamilisha kazi mapema kabla ya Januari 2018 katika Vijiji vyote vya Kata ya Mondo na Mwaniko na kuendelea na Vijiji vingine Wilayani humo ili Wananchi waanze kunufaika na Umeme na kufurahia matunda ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt,John Pombe Magufuli.

Akitoa takwimu na kuelezea dhamira ya Serikali kupitia mradi wa REA,amefafanua kwamba lengo kuu ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2025 Vijiji vyote nchini  takribani 12,378 vitakuwa vimeunganishwa na miundombinu ya Nishati ya Umeme ambapo hadi sasa Serikali imewezesha kupanda kwa asilimia za upatikanaji wa Umeme nchini kutoka asilimia 21% mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 49% kwa sasa na juhudi za kusambaza Umeme vijijini zinaendelea.

Dkt,Kalemani amewataka na kuwaomba Wananchi wa Kata ya Mondo na Mwaniko kutumia fursa hii na kujiorodhesha mapema na kuwa tayari kuwekewa Umeme majumbani mwao kwa gharamaya Tsh,27,000 ambapo katika Wilaya ya Misungwi wanatarajia kuunganisha Wateja zaidi ya 1,568 kwa awamu na Tannesco waendelee kutoa Elimu na kuwahamasisha Wananchi kuweka Wiring katika Nyumba zao hatimaye kuunganisha umeme mapema utakaosaidia na kuwanufaisha kijamii na kukuza uchumi wao kwa kuboresha na kuimarisha shughuli za uzalishaji mali kwa ujumla.

Amemtaka Meneja wa Tanesco Wilaya ya Misungwi kuweka kituo na Dawati la kuwahudumia Wananchi katika Kata ya Mwaniko pamoja na kutoa Elimu kuhusu taratibu na hatua za kufuata ili waweze kupata Umeme kwa gharama nafuu na Wananchi watakaoshindwa waweze kuwekewa Umeme kwa kutumia mtambo wa META kwenye Nyumba za Vyumba vitatu ama vinne.

Waziri Kalemani amewataka Wananchi kuilinda na kuitunza miundombinu ya Umeme  kwa kutoharibu nguzo za Umeme na kuiba mafuta kwenye Transforma zinazowekwa ili iwwze kudumu ma kufanya kazi katika hali ya usalama na utulivu na kuwaonya kwamba atakayejaribu kuharibu miundombinu hiyo Sheria zitachukua mkondo wake .

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Nipo Group Co.Ltd inayotekeleza Mradi huo,Kulwa Delson alisema ataendelea na kazi ya kusambaza Umeme kwa kutandaza nguzo za umeme katika Vijiji vyote alivyopangiwa kwa Mujibu wa Mkataba na kutekeleza kazi kwa kasi na ubora na kuzingatia viwango.

Amesema kwa muda mfupi Kampuni imeweza kusambaza Umeme takribani km.8.9 na kuweza kuunganisha Umeme kwa mteja mmoja na tayari unawaka na wateja wengine wengi wameomba kuwekewa Umeme na kuomba ushirikiano uendelee miongoni mwa Wananchi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.