ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, December 17, 2017

WATU WA TANO WAMEFARIKI DUNIA NA WENGINE KUMI NA TATU KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA MAGARI MAWILI KUGONGANA WILAYANI NYAMAGANA.

¨   
KWAMBA tarehe 16.12.2017 majira ya saa 19:30HRS Usiku katika barabara ya Mwanza - Shinyanga eneo la mtaa wa Buhongwa kata ya Buhongwa wilayani Nyamagana mkoani Mwanza gari namba T 107 BBK Toyota coaster mali ya kampuni ya AUKI WA MWANZA, iliyokuwa ikiendeshw na dereva Badru Habibu (33), mkazi wa Nyegezi Mwanza ikitokea Katoro Geita kuingia Mwanza liligongana na gari lenye namba za usajili T.504 BZB SCANIA lori lenye tela lennye namba T.880 ASA, lililokuwa likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la Salim Omary (28) mkazi wa Dar es salaam likitokea Mwanza kwenda jijini Dar es salaam na kusababisha vifo kwa watu wa tano na majeruhi kumi na tatu wote abiria waliokuwepo kwenye gari hilo aina ya Coaster.

Marehemu waliofariki kwenye ajali hiyo hadi sasa ni mmoja tu aliyetambulika, ambaye ni Abdul Mustafa anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 42 hadi 45 huku marehemu wengine wanne majina yao mpaka sasa bado hayajafahamika.

 Aidha majeruhi wote watatu wapo katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando wakipatiwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri, ambapo pia miili ya marehemu imehifadhiwa hospitalini hapo kwaajili ya uchunguzi na utambuzi.

Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva gari la Coaster aliyekuwa akijaribu kuyapita magari mengine ya mbele bila kuchukua tahadhari kisha kusababisha ajali hiyo iliyopelekea vifo na majeruhi kwa watu.

Madereva wote wa magari hayo wamekamatwa wapo katika mahojiano na jeshi la polisi na pindi uchunguzi ukikamilika wahusika/muhusika atafikishwa mahakamani.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa polisi Ahmed Msangi ametoa wito kwa waendeshaji wa vyombo vya moto hususani madereva wa magari ya abiria kuwa makini pindi wawapo barabarani wakijua wamebeba roho za watu, hivyo wazingatie sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani ili kuepusha vifo na majeruhi ya aina kama hii inayoweza kuepukika makini pindi wanapokuwa barabarani ili kuepuka vifo na majeruhi vya aina kama hii vinavyoweza kuepukika. 

Pia amewataka abiria kutoa taarifa polisi mapema kwa madereva wanaovunja sheria za usalama barabarani ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Aidha Msangi amewaomba wananchi kwenda hospitali ya Rufaa ya Bugando kuwatambua ndugu zao ambao wengine ni majeruhi lakini wengine wamepoteza maisha.

IMETOLEWA NA;
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.