ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 29, 2017

SERIKALI KUJENGA MTAMBO WA KUZALISHA UMEME WA MAJI MTO RUFIJI


Waziri wa Nishati Dr,Medad Kalemani akizungumza na wananchi wa kata ya Mganza wakati wa ziara yake Wilayani Chato ya kukagua utekelezaji wa uwekaji wa umeme vijijini(Rea awamu ya tatu)

Waziri wa Nishati Dr,Medad Kalemani akiwa na makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Chato (Kulia)wakati alipokuwa akizungumza na wananchi.

Mkuu wa wilaya ya Chato ,Shaaban Ntarambe akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nyang’homango wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati kwenye Wilaya hiyo.


Wananchi wa kijiji cha  Nyang’homango wakimsikiliza Waziri wa Nishati  wakati wa ziara yake ya kikazi.

Waziri wa Nishati,Medad Kaleman na Mkuu wa Wilaya ya Chato wakikagua kituo cha afya cha Kata ya Mganza wakati wa ziara yake ya kikazi Wilayani Chato.


Na,Joel Maduka,Chato



Serikali inatarajia kujenga mradi mpya wa kuzalisha umeme  wa maji wa mega watt 2100 kwenye maporomoko ya mto Rufiji ambao utasaidia kuimalisha  miundombinu ya umeme na upatikanaji wa uhakika kwa wananchi.


Akizungumza wakati wa ziara ya siku moja ya  kikazi Wilayani Chato Mkoani Geita ilikuwa na lengo la kukagua na kujionea miundombinu ya umeme wa Rea  awamu ya tatu ,Waziri wa Nishati ,Dr Medadi Kalemani ,alisema kuwa hali ya umeme inaendelea kuimarika siku hadi siku na kuna maeneo mengi yameanza kupata umeme wa kutosha.


“Hapo Nyuma mwezi Novemba tulikuwa tunajitahidi kukarabati mahali ambapo kulikuwa na ubovu wa mitambo lakini kwa sasa hali inaendelea vizuri maeneo mengi ya nchi yetu yanapata umeme kwa wingi  na  tunaanza kujenga mradi mpya wa kuzalisha umeme wa maji wa  mega watt 2100 kwenye maporomoko ya mto Rufiji  ambao utasaidia kuimalisha  miundo mbinu ya umeme na upatikanaji wa umeme hapa nchini”Alisema Kalemani.


Aidha Dr,Kaleman  amewasisitiza wananchi kutoa taarifa kwenye maeneo yao pindi kunapotoakea tatizo na kwamba wateja ambao wamelipia umeme kwa mwaka 2017 ni vyema Tanesco wakahakikisha wanawaunganishia umeme haraka iwezekanavyo kwani mwaka 2018 haitakiwi  kuwepo kwa mteja ambaye ajaunganishiwa  huduma hiyo.


Kalemani ameendelea kutoa wito kwa watendaji wa Tanesco kuhakikisha katika kipindi hiki cha msimu wa siku kuu ya chrismas na mwaka mpya kuimarisha  utoaji wa umeme na uimalishaji wa miundombinu na kufanya patoro ya mara kwa mara kwenye maeneo ambayo kuna shida ya umeme na kwamba suala hilo sio kwenye msimu wa siku kuu tu ni wakati wowote hule kuhakikisha umeme unakuwepo kwenye maeneo ya wananchi.


Elias Mahona ni mkazi wa Kata  Mganza amesema kuwa endapo kama umeme utafika kwenye maeneo ya vijiji utafungua uwigo mpana wa ajira za kujiajiri kwani kwasasa vijana wengi wamekuwa wakikimbilia mijini kutokana na ukosefu wa ajira hivyo umeme utaweza kufungua mirango ya kujiajiri kwa vijana wengi.


Bi,Zawad Nashoni  mkazi wa kijiji cha Nyang’homango amemuomba waziri wa nishati kusaidia umeme uweze kufika kwa haraka zaidi kwenye maeneo yao kwani wamekuwa wakipata shida kutokana na kukosa umeme kwenye maeneo hayo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.