ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, December 10, 2017

PALE JPM ANAPOVUTIWA NA KIATU CHA MAGEREZA.

TANZANIA YA VIWANDA. @GsengoTV

Baba Jesca, Le  president de Tanzanie, Mzee Fulangenge  @officialjohnpombemagufuli #HapaKaziTu  kavutiwa na ndula ya Mrakibu msaidizi wa Magereza Melkior Komba, kitu (made in Tanzania) toka jeshi la magereza Karanga Moshi mkoani Kilimanjaro. #9/12/2017#Nguzaviking#Papii#siku ya uhuru wa kweli  Wafungwa 8157. Jumlisha 61 wa kunyongwa. .

Ni mwaka 2017/9/ December yenye historia. - CC:-@jembenijembe @gijegije @eddievied @mansourjumanne @gsengotv @deejaykflip @harith_jaha @prince_nzwalla @congotoglobal @jonesdgd = #tanzania

RAIS ATIA SAINI NYARAKA ZA MSAMAHA ALIOTOA KWA WAFUNGWA 61 WALIOHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA
Rais John Magufuli ametia saini nyaraka za msamaha alioutoa kwa wafungwa 61 waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa na wawili Nguza Viking (Babu Seya) na Johnson Nguza (Papii Kocha) waliohukumiwa kifungo cha maisha jela.

Rais Magufuli ametia saini nyaraka hizo leo Jumapili Desemba 10,2017 Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Msamaha huo aliutoa jana Jumamosi Desemba 9,2017 katika maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika (Tanzania Bara).

Rais Magufuli amelipongeza Jeshi la Magereza kwa kazi nzuri ya kurekebisha tabia za wafungwa.

Taarifa ya Ikulu imesema Rais Magufuli amesisitiza kuwa pamoja na kutolewa msamaha huo, vyombo vya dola viendelee kusimamia sheria.

Amelitaka Jeshi la Magereza kuhakikisha linawatumia wafungwa kuzalisha mali, yakiwemo mazao ya kilimo na kufanya kazi za ujenzi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.