ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 2, 2017

WALIMU WATAKIWA KUTUMIA FURSA YA UJASIRIAMALI KWAAJILI YA KUJIINUA KIUCHUMI.

Walimu wa wilaya ya Geita wakiwa kwenye  Kikao cha kujadili maendeleo na changamoto ndani ya chama cha walimu Wilaya ya Geita.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya  Mji wa Geita ,Leornad Kiganga Bugomola akizungumza na Walimu wakati wa kikao hicho uku akiwasisitiza kuendelea kufanya kazi kwa kujituma na pia aliwapongeza kwa kuweza kufanya vizuri kufikia hatua ya Mkoa kuchukua nafasi ya Pili kwenye mtihani wa darasa la saba Kitaifa.
Katibu wa chama cha Walimu Wilaya ya Geita,John Kifimbi akisoma risala kwa Mgeni rasmi.
Baadhi ya wageni waalikwa ambao wanatoka taasisi mbali mbali wakifuatilia kikao hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akitoa vyeti kwa walimu ambao wamefanya vizuri ndani ya chama hicho.

Mwenyekiti wa chama cha walimu(CWT)Wilaya ya Geita,Alfred Alexander akiwasisitiza walimu kuendelea kuwa na mshikamao ndani ya chama hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akiwasisitiza walimu kujingea tabia ya kuwa na vitega uchumi mbali mbali kwenye mazingira ambayo wanafanyia kazi.

                                                      (PICHA NA JOEL MADUKA)

Walimu Wilayani Geita wametakiwa kutumia nafasi walizonazo katika kujiinua kiuchumi kwa kuwekeza kwenye Shughuli za ujasiriamali.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Geita,wakati wa Mkutano mkuu wa chama cha Walimu (CWT)Wilaya ya Geita ambao  umefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Mji lengo likiwa  kuangalini ni kipi chama kimefanya ndani ya miaka Miwili.

 alisema kuwa  wakati umefika kwa walimu kuwekeza katika fursa za ujasiriamali na kutokuogapa kukopa na kwamba kama kuna mtu ambaye anampiga vita mwalimu kuwekeza na huku anatekeleza majukumu yake ya msingi ni sawa na kutokumtendea haki.

“Lengo la kuandaa vitega uchumi kabla ya uzee na manufaa ya uwekezaji ni kwa manufaa ya jamii kwa hiyo walimu kama kuna mtu anakupiga vita kwa ajili ya uwekezaji na unafundisha kwa wakati sahihi mtu huyo nipeni taarifa”Alisema Kapufi.

Mwenyekiti wa chama cha walimu Mkoani Humo,Mwl Lusato Zabron Mashauri ,ameelezea kuwa hali ya kiuchumi bado ni mbaya kwa walimu hususani wale ambao wanaishi vijijini wengi wao wamekuwa wakishindwa kufanya biashara kutokana na viongozi wengi wa kisiasa kutokuwa na uelewa juu ya haki za walimu.

“Hali ya kiuchumi kwa walimu hairidhishi hususani wale ambao wanaishi vijijini kwani wengi wao wamekuwa wakipigwa vita na viongozi wa kisiasa mwalimu anapojaribu kuinuka kiuchumi anapigwa vita na viongozi ao”Alisema Lusato.

Kemilembe Gerigori ambaye anawawakilisha walimu wanawake Mkoani Humo,alisema hali ya mazingira ya walimu ni magumu kutokana na namna ambavyo wamebanwa katika suala la muda wa masomo hivyo wengi wao wamekuwa wakishindwa kujishughulisha na ujasiriamali kwa kukosa muda.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.