ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 17, 2017

TANZIA: ALIYEKUWA KATIBU MKUU (CWT) AFARIKI DUNIA.



Dar es Salaam. Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Yahya Msulwa amefariki dunia jana katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Katibu mkuu wa zamani wa chama hicho, Gratian Mkoba ameithibitisha Mwananchi leo Ijumaa Novemba 17 wakati akizungumza kwa simu.

Mkoba amesema, “Ni kweli amefariki jana usiku na alipelekwa jana hiyo usiku kwa mujibu wa ndugu zake walionipa taarifa, maana mimi nilikuwa nina wiki moja hatujawasiliana na sijui alikuwa na anasumbuliwa na nini,”amesema Mkoba.

Amesema hivi sasa yupo njiani kwenda nyumbani kwa marehemu Tuangoma kujua taratibu za mazishi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.