ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 2, 2017

MKUU WA MKOA WA PWANI INJINIA EVARIST NDIKILO AWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA KIWANDA CHA KUTENGENEZEA CHAKI KISARAWE

 
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo akizungumza na wananachi na baaadhi ya viongozi mbali mbali wa serikali mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika kiwanda hicho cha chaki cha Mkongoma kiichopo Wilayani Kisarawe. (PICHA NA VICTOR MASANGU)

Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha chaki Geofrey Mkongoma akitoa risala fupi  kwa mgeni rasmi mara baada ya  kiwanda hicho kuwekea jiwe la msingi na Mkuu wa Mkoa wa Pwani .

 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Happines Seneda akizungumza na wananchi waliofika katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi katika kiwanda hicho cha chaki.

Baadhi ya viongozi wa halmshauri ya Wilaya ya Kisarawe wakiwa katika halfa hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi katika kiwanda hicho cha chaki.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)

NA  VICTOR  MASANGU, KIRASAWE

KATIKA kuunga mkono juhudi za Rais wa serikali ya awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli katika kuwa na uchumi wa viwanda,Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo amewataka wawekezaji wote kuhakikisha wanaachana kabisa na tabia ya kukwepa kulipa kodi  na badala yake watimize wajibu wao ipasavyo bila ya kuvunja sheria na taratibu za nchi ili kuweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wananchi.

Injinia Ndikilo ametoa kauli hiyo wakati  wa halfa ya uwekaji wa jiwe la msingi katika kiwanda cha chaki kinachoendelea kujengwa katika awamu ya kwanza katika kijiji cha Msanga zalala kata ya Msimbu Wilayani Kisarawe na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa , serikali, madhehebu ya dini pamoja na watendaji wa  serikali za vijiji na vitongoji.   

Pia Mkuu huyo alibainisha kuwa katika uwekezaji wa viwanda katika Mkoa wa Pwani baadhi ya maeneo bado yanakabiliwa na changamoto ya kutokuwa ni nishati ya umeme wa uhakika pampja na kuwepo kwa mioundimbinu mibovu ya barabara hivyo ameagiza mamlaka zote zinazohusika kulifanyia kazi suala hilo ili kuweza kuwavutia wawekezaji wengine.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe  Happiness Seneda alitoa wito kwa wananchi wengine kutumia fursa zilizopo katika kujifunza mambo mbali mbali ya ujasiriamali  na kuanzisha viwanda vidogo vidogo kwa lengo la kuweza kuunga juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kuwa na uchumi wa kati pamoja na kuwapa nafasi zaidi wawekezaji ambao ni wazawa ili waweze kutoa fursa za ajira kwa vijana.

Awali  Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda hicho cha chaki Geofrey Mkongoma  akisoma taarifa yake ameiomba serikali ya awamu ya tano  kuweza kuwapa fursa  ya kipekee wazawa  wa  Tanzania katika   suala zima la uwekezaji  wa ujenzi wa viwanda  vidogovidogo huku akitaja akisema changamoto kubwa ni suaala la umeme wa uhakika.

Alisema kuwa lengo lake kubwa ni kuhakikisha anaunga mkono juhudi za serikali ya wamu ya tano katika kuwa na uchumi wa viwanda hivyo ataendelea kushirikiana bega kwa began a wadau wengine kwa lengo la kuweza kufanikisha malengo aliyojiwekea ya kuweza kutoa fursa za ajira kwa wazawa pamoja na kuongeza uzalishaji wa chaki.

“Hiki kiwanda kilianza tangu mwaka 2013 na kwa sasa kama mnavyoona  mimi nimeshaajiri wafanyakazi wapatao 38. Ambao ninawalipa kutokana na kiwanda hiki cha chaki hivyo kitu kikubwa ninachokiomba kwa serikali ni kutoa sapoti kubwa zaidi kwa wawekezaji ambao ni wazawa ili waweze kuendelea kujenga viwanda vidogo vidogo ili kuweza kukuza uchumi wa nchini,”alisema Mkurgenzi Mkongoma.

Nao baadhi ya wakinamama ambao wanafanya kazi katika kiwanda hicho cha chaki  akiwemo  Tedy Mzingula na Shoboa Msagasa wamesema kuwa kipato wanachokipata kinaweza kuwabadilisha kwa kiasi kikubwa katika suala zima la kujikwmau kimaisha kutokana na kuendesha familia zao ikiwemo kuwasomesha watoto walionao pamoja na kuwahudumia mahitaji madogo madogo.

“Sisi kwa kwli kama wafanyakazi wa kiwanda hiki tunapenda kumshukuru Mkurugenzi wetu kwa kuweza kupenda katika hali na mali, na kutokana na kufanya kazi hii fedha ambayo tunaipata inatusaidia kwa kiasi kikubwa katika kuendesha familia zetu, kwani wengne tuna watoto ambao tunawasomesha na maisha yanaendelea lakini kikubwa ni serikali kumsaidia kuweza kupata umeme,”walisema.

KIWANDA hicho cha chaki ambacho kinajulikana kwa jina la  Mkongoma Chalk Factor kilianzishwa mnamo mwaka 2013 ambapo kwa sasa kina jumla ya wafanyakazi zaidi ya 38 wakiwemo vijana pamoja na wakinamama kutoka maeneo mbali mbali ya Wilaya hiyo ya Kisarawe.
     

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.