ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 20, 2017

KAMPUNI ITAKAYO NUNUA PAMBA CHAFU KUKIONA CHA MTEMA KUNI.

KATIKA juhudi za kufikia malengo ya mapinduzi ya viwanda kupitia zao la Pamba, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Agrey Mwanri amezifuta likizo zote kwa maafisa Ugani na wadau wote wanaohusika na ugawaji mbegu kwa wakulima kipindi hikicha msimu wa kilimo 2017-2018.

Mwanri ametoa agizo hilo jana katika uzinduzi wa msimu mpya wa kilimo cha pamba uliofanyika kitaifa katika Kijijicha Mwamashimba wilayani Igunga Mkoani Tabora na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa zao hilo kutoka mikoa ilimayo zao la pamba hapa nchini .

Amesema haoni sababu za kukesha mwaka mzima wakifundisha manna ya kilimo cha kisasa na kuhubiri mapinduzi ya kilimo chenye manufaa kwa zao la pamba kisha ukafika msimu wa kilimo nao wataalamu na wagawaji pembejeo wakikimbia majukumu yao kwa kisingizio cha likizo, hilo hato kubaliana nalo. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA 



Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Agrey Mwanri akitia msisitizo kwa mmoja ya maagizo yake, katika sherehe za uzinduzi wa msimu wa Kilimo bora cha Pamba 2017/2018 Kanda ya Magharibi zilizofanyika katika kijiji cha Mwamashimba wilayani Igunga mkoani Tabra.
BOFYA PLAY 
Igunga, 20 Novemba, 2017: Msimu mpya 2017/18 wa kilimo cha pamba katika Kanda ya Magharibi inayojumuisha mikoa ya Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Geita, Tabora, Mara, Kagera, Singida, Kigoma na Katavi, umezinduliwa rasmi jana ambapo upandaji pamba umeanza rasmi na utaendelea hadi mwishoni mwa mwezi Desemba.
Akiongea katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania (TCB), Marco Mtunga amesema kwamba katika msimu wa kilimo wa 2017/18 jumla ya tani 25,000 za mbegu zimetengwa zikijumuisha tani 11,548 za mbegu mpya ya UKM08 na tani 13,452 za mbegu ya UK91. Kiasi hiki kinawahakikishia wakulima uwepo wa mbegu za kutosha kwa maeneo yote yatakayozalisha pamba msimu wa kilimo. 
 BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.


 Hadi tarehe 12 Novemba 2017, jumla ya tani 11,056 ambayo ni sawa na asilimia 70 ya mbegu zote zimesambazwa katika maeneo mbalimbali kati ya tani 15,694 zilizopangwa kusambazwa katika mgao wa awali. Zoezi la usambazaji wa mbegu lilianza tarehe 15 Septemba 2017 na limepangwa kukamilika tarehe 30 Novemba 2017.

Jumla ya ekari milioni moja na laki tatu zinatarajiwa kupandwa pamba msimu wa kilimo 2017/18. Serikali kwa kushirikiana na Wadau imefanikiwa kufufua mfumo wa kuzalisha mbegu bora za kupanda na kwamba azma ya Serikali ya kuwapatia wakulima mbegu bora mpya ya UKM08 ifikapo mwaka 2018/2019 itatekelezwa kama ilivyopangwa.
 Aliongeza kusema kwamba; Mfumo wa uzalishaji wa mbegu bora za pamba unaanzia Kituo cha Utafiti cha Ukiriguru ambapo mbegu mama (Breeder Seeds) inazalishwa na baada ya kupatikana zinapelekwa kupandwa katika shamba la Nkanziga lililopo Wilayani Misungwi ili kuzalisha mbegu za awali (Pre-Basic Seeds). Baada ya hapo mbegu zinapelekwa kuzalishwa na wadau wengine (Quton seed Co. na Gaki ginnery) katika Kata ya Mwabusalu wilayani Meatu ili kupata mbegu za Msingi (Basic Seeds).Ngazi ya mwisho ya katika mtiririko wa uzalishaji wa mbegu iliyothibitishwa (certified seeds) zinazalishwa wilayani Igunga. Katika msimu wa kilimo wa 2017/18, jumla ya tani 11,548 za mbegu mpya ya UKM08 zinasambazwa katika Wilaya 34 kati ya 48 zinazolima pamba nchi nzima.

Kwa lengo la kuboresha kilimo cha pamba Serikali imejipanga kueneza matumizi ya mbegu zilizoondolewa nyuzi ili kwenda sambamba na mataifa mengine yanayolima duniani kwani kilimo cha pamba duniani kinafanyika kwa kutumia mbegu zilizoondolewa nyuzi. Katika msimu huu wa kilimo wa wa 2017/18, Mikoa ya Tabora na Mara inapanda mbegu zilizoondolewa nyuzi na kwamba elimu ya matumizi ya mbegu hizi inaendelea kuenezwa katika maeneo yote.  Lengo la Serikali ni kuwapatia wakulima wote mbegu zilizoondolewa nyuzi ifikapo msimu wa kilimo wa 2018/19.  Zifuatazo ni faida za Mbegu zilizoondolewa nyuzi:-
• Kuua vimelea vya magonjwa na wadudu hivyo kuzuia kuenea kwa magonjwa
• Mbegu zinatumika kidogo.
• Gharama kidogo za usafirishaji, utunzaji.
• Uwezekano wa kutumia mashine katika upandaji.
• Uhakika wa uotaji kwa kuwa mbegu zisizokomaa, zilizoshambuliwa na wadudu zinaondolewa.
• Ni rahisi kuchanganya na kiuatilifu na kusafisha kwa kuwa inanyumbulika.
Tatizo la pamba Tanzania si bei wala soko bali ni tija ndogo ya kilo 300 kwa ekari badala ya kilo 1,000 kwa ekari ambazo wakulima bora wa pamba wanazalisha kwa sasa. Mkulima wa pamba ataweza kuongeza kipato chake mara mbili au mara tatu akiongeza tija. Ili kubadilisha hali hii, Bodi ya Pamba na Serikali kwa ujumla inachukua hatua zifuatazo:

(i) Kueneza kilimo cha mkataba ili wakulima waweze kupata pembejeo za kutosha kwa mkopo ili asiyekuwa na uwezo wa kujinunulia pembejeo asikwame kulima pamba;
(ii) Kufufuliwa kwa mfumo wa kuzalisha mbegu kunawezesha wakulima kupanda mbegu bora zilizothibitishwa na hivyo kuongeza tija
(iii) Mheshimiwa Waziri Mkuu na Waziri wa TAMISEMI wametoa maelekezo mahsusi kuhusu usimamizi wa shughuli za zao la pamba katika ngazi zote hususani utoaji wa huduma za ugani.
(iiii) Aidha wakulima wawezeshaji 4,532, wawili kutoka kila kijiji kinacholima pamba wameainishwa na wanaunganishwa na mtandao wa wagani ili mashamba yao yatumike kama shamba darasa. Wakulima wawezeshaji (Lead Farmers) wanazalisha kilo kati ya 800 na 1,200 kwa ekari.
(v) Serikali imenunua na kusambaza kamba za kupandia katika Wilaya 13 ambazo zimekithiri katika upandaji wa pamba kwa kusia na mafunzo yanaendelea kutolewa
Kauli mbiu tasnia ya pamba ni “MKULIMA KUTOKA MAFURUSHI MATATU HADI MAFURUSHI KUMI KWA EKARI” maana yake kutoka kilo 300 hadi kilo 1,000 kwa ekari.

“Wakati sasa umefika wa kila mkulima wa pamba nchini kulima kwa tija ili kuongeza uzalishaji na kujikwamua kutoka kwenye umaskini kwani katika uzalishaji wa zao la pamba tija inachangiwa na kuzingatia kanuni za kilimo bora cha pamba na kupanda mbegu bora. Iwapo mkulima atapanda pamba kwa mistari na kuzingatia nafasi inayopendekezwa na wataalam ambayo ni sentimita 90 kutoka mstari hadi mstari na sentimita 40 kutoka shimo na shimo, mkulima atajihakikishia kuwa na idadi ya miche isiyopungua 22,222 kwa ekari ambayo itamwezesha kupata si chini ya kilo 1,000 za pamba mbegu.
Kupanda pamba kwa wakati na kwa nafasi inayopendekezwa ni kigezo kikubwa cha kupata pamba nyingi na bora, lakini mkulima unatakiwa uzingatie kanuni zingine katika mtiririko wa kanuni kumi za kilimo bora cha pamba ambazo ni pamoja na kupalilia pamba mara kwa mara, kupunguza miche iliyozidi kwenye shamba, kunyunyizia viuadudu kudhibiti visumbufu vya mimea, kuvuna kwa wakati na kutenga pamba katika madaraja ya A na B na mwisho kung’oa na kuchoma moto masalia yote ya pamba baada ya kumaliza kuvuna.



















Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.