ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, October 22, 2017

MONGELA APIGA BITI KALI WAKUU WA WILAYA NA WAKURUGENZI HALMASHAURI ZINAZOLIMA PAMBA MKOANI PAKE

NA. ZEPHANIA MANDIA G.SENGOBLOG TV


Wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri zinazolima zao la pamba mkoani Mwanza wametakiwa kuacha mzaha na makapuni yanayoweka mkakati wa kutaka kuhujumu zao la pamba kwa musimu 2017 /2018



Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella amesema hayo katika kikao cha kuweka mkakati wa kilimo cha Pamba mkoani Mwanza



Katika hatua nyingine mkuu huyo amewaagiza wakuu hao wa wilaya kutoingia mikataba ambayo inaweza kudhofisha kilimo cha pamba



Awali Mkuu wa idara ya kilimo wilayani Magu  Godleda Masale akitoa taarifa ya maadalizi ya kilimo kwa musimu huu 2017 /2018 amesema kuna mkakati wa kuongeza uzalisha kutoa kilo 300 kwa hekta moja  mpaka 800 kwa msimu huu



Baadhi ya wakuu wa wilaya zinazolima pamba mkoani mwanza wamesikitishwa na kitendo cha bodi kwa kusitisha kilimo cha mkataba na baadhi ya makapuni ya kusambaza  mbengu kushindwa kufikaia malengo 



Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya PambaTanzania  Gabriel Mwalo amesema kuwa bodi itahakikisha wakulima wote wanapata mbengu kwa wakati pamoja na pembejeo hata  wale ambao hawapo kwenya  kilimo cha mkataba.


Kikao hicho kimewashirikisha wakuu wa wilaya zinazolima zao la pamba wakurugenzi na wakuu wa idara  kikiwa kimeangazia kilimo cha mkataba ubora wa mbengu na kuweka mkakati wa kuhakikisha wanafikia malengo ya kilo milioni  32 katika msimu wa mwaka 2017/2018.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.