ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 20, 2017

TADB YAJADILIANA NA BENKI YA MAENDELEO YA CHINA NA MFUKO WA MAENDELEO YA AFRIKA WA CHINA

Katibu Mkuu wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati wa Kikao cha Pamoja kati wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na Mfuko wa Maendelo ya Afrika wa China (CADFUND) kilichofanyika Shangrila Hotel, Guangzhou China juzi. Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB Bwn. FRANCIS Assenga na kulia kwake ni Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki na Afisa Ubalozi wa Tanzania nchini China Bwn. Lusekelo Gwassa.

PICHA YA PAMOJA ya baadhi ya Washiriki wa Kongamano la Ushiriani wa Biashara na Uwekezaji kati ya China na Tanzania likilofanyika Guangzhou China Oktoba 2017. Katikati ni Katibu Mkuu wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Prof.  Adolf Mkenda aliyekuwa Mgeni Rasmi wa Kongamano hilo, kulia kwake ni. Mhe. Adam Kimbisa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki; Katibu Mkuu wa Biashara Viwanda na Masoko wa Zanzibar Bw. Juma Alli Juma; Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki; na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Sekta Binafsi (TPSF) Bw. Akaro. Kulia kabisa aliyesimama ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Tanzania (TADB) Bw. FRANCIS Assenga.

Baadhi ya Washiriki wa Kongamano la Biashara, Viwanda na Uwekezaji lililofanyika Guangzhou China Oktoba 2017 wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi wa Kongamano hilo Pro. ADOLF Mkenda (Katibu Mkuu wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji anayeshughulikia Uwekezaji. Wa pili kushoto kwa Prof. Mkenda ni Bwn. FRANCIS Assenga, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB na kulia kabisa wakiokaa ni Bwana Du Chuan, Mkurugenzi wa Biashara ya Mihogo wa Shirika la Sinolight International Holdings la China linayojishughulisha na uzalishaji na uagizaji wa mihogo toka nje.

Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bwn. FRANCIS Assenga; Katibu Mkuu wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Bwn. ADOLF Nkenda; Makamu Rais na Naibu Mtendaki Mkuu wa CADFUND Bwn. Wang Yong na Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki, mara baada ya kumalizika kwa kikao cha pamoja
Ujumbe wa Tanzania wakiwa kwenye Picha ya Pamoja na Makamu Rais wa Mfuko wa Maendeleo ya Africa wa China 'CADFUND".
Na Mwandishi wetu,
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imefanya mazungumzo na Taasisi mbili muhimu za kifedha na kiuchumi nchini China kwa ajili ya upatikanaji wa fedha za uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu na viwanda nchini Tanzania hususan kwenye Sekta ya Kilimo.

Majadiliano hayo yalifanywa kati ya Ujumbe wa TADB ulioongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki , Bw. Francis Assenga alipokutana na Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya China (CBD) kwenye Mkutano uliofanyika Shangrila Hotel, Guangzhou China wakati wa Kongamano la Pamoja la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na China.

Pande zote mbili zilikubaliana kuendelea na kuimarisha ushirikiano  utakaowezesha kupatikana kwa fedha kwenye uwekezaji wa miundo mbinu ya kilimo na viwanda vidogo vidogo vya uongezaji thamani kwenye mazao ya kilimo kwa wakulima nchini.

Katika ziara hiyo TADB pia ilifanya  majadiliano ya kina na Mfuko wa Maendeleo ya Africa wa China (China African Development Fund) ambao hufanya uwekezaji mkubwa wa miradi ya maendeleo na ya kibiashara (Equity investmenta) kwenye nchi za Afrika ikiwemo Tanzania.

Mazungumzo hayo yalihudhuriwa na Ujumbe wa ulioongozwa na Makamu Mtendaji wa Rais na Naibu Mtendaji Mkuu wa 'CADFUND' Bwn. Wang Yong aliyefuatana na Mkurugenzi Mkuu wa Sekta ya Viwanda, Kilimo, Afya na Uwekezaji, Bw. Lei Ma; Mkurugenzi Mkuu wa Maendeleo ya Masoko na Huduma Elekezi Bw. Henry Liu; na Meneja wa Uwekezaji wa Viwanda, Ardhi na Kilimo Bw. Luo Zhongquan.

Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Katibu Mkuu wa Viwanda Biashara na Uwekezaji (UWEKEZAJI), Prof. Adolf Mkenda. Wengine waliohudhuria ni Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki; na Afisa Ubalozi wa Tanzania nchini China Bw. Lusekelo Gwassa.

Katika mazungimzo hayo, pamoja na mambo mengine CADFUND walikubali kuendelea kutoa fedha kwenye miradi ya kiuchumi na uwekezaji mkubwa kwenye nyanja kuu nne zikiwemo kilimo; viwanda; madini; na miundombinu kama ya maji na umwagiliaji.

Aidha CADFUND na TADB ziliainisha maeneo kadhaa ya ushirikiano kama vile Uhakiki na Usimamizi wa miradi; Utafiti; Ukaguzi; na Ujengaji wa Uwezo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.