ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, October 17, 2017

SERIKALI YA IRELAND YAWEKEZA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 700 KUPAMBANA NA UKATILI WILAYANI MISUNGWI

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland anayeshughulikia Maendeleo, Ciaran Cannon akikata utepe wa moja ya vijarida vya uelimishaji kama ishara ya uzinduzi wa Mradi wa Mpango wa kupambana na ukatili wa jinsia, uliofanyika kwenye viwanja vya Amani wilayani Misungwi, Mwanza, kushoto ni mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.
"Ndiyo hiki"..........!
Oyeeeeeee......!!
Yaliyomo yamo?
Balozi wa Ireland nchini, Paul Sherlock naye akizawadiwa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland anayeshughulikia Maendeleo, Ciaran Cannon akizungumza kwenye uzinduzi wa Mradi wa Mpango wa kupambana na ukatili wa jinsia, uliofanyika kwenye viwanja vya Amani wilayani Misungwi, Mwanza, kushoto ni mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.
SERIKALI ya Jamhuri ya Ireland kupitia Shirika la Maendeleo nchini humo limetoa msaada wa kiasi cha Uero 350,000 (zaidi ya milioni 700) kwa Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Watoto (Kivulini) mkoani Mwanza kwa ajili ya kuwezesha mpango wa kujenga uwezo wa jamii na taasisi za Serikali ili kuendelea kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia katika Kata 10 wilayani Misungwi mkoani hapa.

Msaada huo umetolewa leo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland anayeshughulikia Maendeleo, Ciaran Cannon,  aliye ambatana na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Maendeleo nchini humo, Ruairi De Burca pamoja na Balozi wa Ireland nchini, Paul Sherlock, kwenye uzinduzi wa Mradi wa mpango wa kupambana na ukatili wa jinsia, uliofanyika kwenye viwanja vya Amani wilayani Misungwi.

Kata zilizo nufaika na mradi huo ni pamoja na Usagara, Idetemya, Kolomije, Igokelo, Misungwi, Mbarika, Misasi, Nundulu, Sumbugu na Mabuki walengwa watakaofikiwa moja kwa moja  144,744 na wengine 289,488 ambao watafikiwa kwa kupata elimu kutoka kwa wananchi wengine waliopata mafunzo.

Mwanamke mmoja kati ya saba nchini Tanzania amebainika kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia, hatua  ambayo inazidi kuchangia kupunguza nguvu kazi ya taifa.


Waziri huyo wa Mambo ya nje wa Ireland, Bwana Cannon amesema kuwa serikali ya nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika mambo mbalimbali ikiwemo kupambana na vitendo vya Ukatili, Afya na Mfuko wa kusadia kaya masikini nchini (TASAF) ili kuleta mabadiliko katika Nyanja ya Uchumi. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akifunguka mbele ya wananchi na kusanyiko.
Zaidi ya asilimia 40 ya Wanawake nchini (Tanzania) wamebainika kukumbwa na vitendo vya ukatili, hali ambayo haiwakumbi wanawake pekee bali pia wanaume, nao wameripotiwa kukumbana na vitendo hivyo vya ukatili nazo takwimu zikishindikana kupatikana ipaswavyo kutokana na wanaume hao kuona kama ni suala la aibu na fedheha kuripoti kwamba wametendewa ukatili.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amewaonya watu wanaojihusisha na vitendo vya ukatili akisema kuwa serikali haitosita kuchukuwa hatua kali kwa wahalifu hao. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA
Yasini Ally.



Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kivulini, Yasini Ally amema Wilaya Misungwi ilikuwa ikikabiliwa kiwango cha kutisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake kunyanyaswa na waume zao ambapo wamepambana  kwa kila hali hatimaye sasa wanashuhudia vitendo hivyo kupungua kwa kasi. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA
 
Awali kabla ya kuzindua mradi huo wa Ukatili wa Kijinsia kwa Wanawake na Watoto unaoendeshwa na KIVULINI Waziri huyo ameshuhudia uzinduzi wa Zoezi la Uhawilishaji fedha katika kijiji cha Misungwi pamoja na kutembelea kituo cha Afya cha Misasi ambapo ameahidi Serikali yake itaendelea kuchangia katika utatuzi wa changamoto zake.

Kwa mjibu wa takwimu za Mwaka 2015/ 2016 zinaonyesha kuwa, vitendo vya ukatili wa kinjisia nchini ni asilimia 58 kitendo ambacho kimetajwa kuwa kinachangia shughuli za maendeleo katika jamii kusuasua.




Ngoma asili.
Jiografia ya eneo la uzinduzi.
Ngoma asili ikichukuwa nafasi kunako kusanyikoni.
Wadau walio na dhamana ya uelimishaji toka KIVULINI wakisikiliza kwa umakini yanayojiri kusanyikoni.
Utambulisho.
Ngoma inogile.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bwilu Girls toka jijini Mwanza nao wameshiriki uzinduzi huo unao husika katika Ku-Chochea Mabadiliko kuleta usawa wa kijinsia.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Maendeleo nchini Ireland, Ruairi De Burca akizawadiwa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland anayeshughulikia Maendeleo, Ciaran Cannon akiselebuka mangoma ya kisukuma sanjari na Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella.
Wanaharakati walipata fursa ya kueleza jinsi gani wanavyo sambaza elimu, shughuli zao, changamoto na ushauri.
Kisha nao wakapewa somo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland anayeshughulikia Maendeleo, Ciaran Cannon.
Dawati la Jinsia toka Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza likifanikisha adhma yake katika usaidizi wa kisheria, uelimishaji, kupambana na udhibiti wa vitendo vya ukatili kwa jamii.
Kivulini is a civil society organisation which works to improve women’s rights in Tanzania . Kivulini advocates for women’s and girl ’s rights in Tanzania by emphasising the prevention of Violence against women against women and girls. 

The Kiswahili word Kivulini means “in the shade”. It implies a place of safety, under a tree or otherwise, where people meet for discussions and offer support to one another. 

Kivulini was established in 1999 to create opportunities for community members to come together, talk, organise and work towards preventing domestic violence so that women and girls are able to enjoy their rights as stipulated in the Constitution of The United Republic of Tanzania, African Charter and various human rights conventions.

Vision

Kivulini’s vision is to see a community free from domestic violence where women’s rights are respected and valued. Kivulini’s mission seeks to achieve this vision by facilitating and enabling social, economical, and legal environment which guarantees women and girls the right to live in violence-free communities through self empowerment, advocacy and building an active social movement for change.

Objectives

Kivulini is committed to facilitate an enabling social, economical, and legal environment which guarantees women and girls the right to live in violence-free communities through self empowerment, advocacy and building an active social movement for change. 

To build momentum for the prevention of Violence Against Women and girls with emphasis on domestic violence against women and girls in the Lake Victoria Regions (Mwanza, Kagera, Mara and Shinyanga) and Singida by:
  1. Mobilizing communities to take action against Domestic violence
  2. Strengthening the capacities of local government and CSOs (including Kivulini)
  3. Advocating and influencing key local and national policies that empower and benefit women and girls.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.