ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 23, 2017

USIKU HUU NA TUZO ZA FIFA 2017.

 England. Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia wa Fifa 2017 baada ya kuwapiku wachezaji Lionel Messi na Neymar katika kipengele hicho.

Tuzo hizo zimetolewa usiku huu (Oktoba 23) ambapo mchezaji huyo aliyeambatana na mpenzi wake na mwanae amewashukuru waliompigia kura kwa kuweza kushinda pamoja na mashabiki na wachezaji wenzake.

“Nashukuru wote mlionipigia kura kwa kunifanya nishinde tuzo hii,” amesema Ronaldo.

Mbali na tuzo hiyo Ronaldo ametajwa katika kikosi bora cha mwaka 2017 ambacho kimewajumuisha Messi na Neymar na nyota wengine akiwemo Sergio Ramos, Toni Kroos, Andres Iniesta, na Dani Alves.

Tuzo ya mchezaji bora wa kike wa Fifa 2017 ilienda kwa Lieke Martens ambaye hakuudhuria katika utoaji wa tuzo kutokana na kujiandaa na kujiandaa na mechi ya kufuzu kombe la dunia la wanawake.

Ukumbi ulilipuka kwa shangwe wakati linatangazwa goli bora la mwaka ‘Puskas’ ambapo katika magoli 10 bora mashabiki walisikika wakimtaja nyota wa Arsenal, Olivier Giroud ambaye alitangazwa kama mshindi.

Wengine walioshinda tuzo za Fifa 2017 ni Zinedine Zidane (Kocha bora kwa waume), Sarina Wiegman (kocha bora kwa wanawake) Gianluigi Buffon (Kipa bora), Mashabiki wa Celtic (Kikundi bora), Francis Kone (Mchezo wa kiungwana).

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.