ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 2, 2017

WANAFUNZI 7 WAFARIKI KATIKA MOTO ULIOCHOMA BWENI KENYA.

Maafisa wa polisi wakishika doria nje ya shule ya Moi Girls liliopo jijini Nairobi nchini Kenya Wanafunzi saba wamefariki na makumi wengine wakijeruhiwa baada ya moto kuchoma bweni la shule ya Moi Girls mjini Nairobi.

Waziri wa elimu Fred Matiang'i amesema kuwa wanafunzi wengine 10 walijeruhiwa na wamelazwa hospitalini.

Wawili kati ya 10 wako katika hali mbaya ,kulingana na madaktari huku wengine wanane wakiwa hawako katika hali mbaya.

Parents and some students at Moi Girls School

Wazazi na baadhi ya watoto wa shule ya Moi Girls mjini Nairobi wakifarijiana kwenye eneo la tukio.
 
Takriban wanafunzi 10 wamerodheshwa kuwa hawajulikani waliko kulingana na kitengo cha habari cha maafisa wa msalaba mwekundu katika shule hiyo.


Kenya Red Cross personnel attend to a woman who
Wafanyakazi wa chama cha msalaba mwekundu wakimsaidia mama aliyezimia mara baa ya tukio la kufariki watoto shule ya Moi Girls mjini Nairobi. 
 
Matiang'i amesema kuwa shule hiyo imefungwa kwa wiki mbili huku uchunguzi ukianzishwa kuhusiana na sababu ya moto huo.

Waziri huyo hatahivyo amesema kuwa wanafunzi wa kidato cha nne wataendelea na masomo yao ifikiapo siku ya Ijumaa na watasaidiwa kuendelea na masomo yao wakati ambapo wanajianda kufanya mtihani wa kidato cha nne wa KCSE.

Amesema kuwa kundi la wataalam wa upasuaji ikiwemo madaktari wako katika shule hiyo kubaini chanzo cha moto huo.

Amesema kuwa mkuu wa shule hiyo amewataka wazazi kuwachukua wanawao.

Relatives of students at Moi Girls School
Ndugu jamaa  wa wanafunzi wa Moi Girls School Nairobi wakitokwa na machozi baada ya kufariki kwa wanafunzi hao 7 huku wengine 10 wakiwa majeruhi.
 
Bwana Matiang'i aliandamana na gavana wa Nairobi Mike Sonko.

Kulingana na gazeti la Daily Nation nchini humo mwanafunzi mmoja wa kidato cha kwanza ambaye alikuwa miongoni mwa wale waliotibiwa baada ya kisa hicho alisema kuwa moto huo ulianza mwendo wa saa saba usiku.

Alisema kuwa bweni lililochomeka lilikuwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza na kwamba kulikuwa na makelele ya wanafunzi waliojaribu kujinusuru mbalii na mkanyagano huku wasichana wakijaribu kutoka ndani ya bweni hilo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.