ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, September 18, 2017

RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA AJALI YA WATU 13 UGANDA.



 NA: GSENGO BLOG
Watu 13 wamepoteza maisha na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea Katonga wilayani Mpiji nchini Uganda.

Ofisa wa polisi wa Katonga, Philip Mukasa amesema ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Jumatatu ikihusisha basi aina ya Toyota  Coaster lililogongwa na lori.

Mukasa amesema basi lililohusika katika ajali hiyo lina namba ya usajili ya Tanzania na lori lina namba za Uganda.

Amesema lori lililokuwa katika mwendokasi lilipasuka gurudumu hivyo kuyumba na kugonga gari hilo la abiria.

Wakati huo huo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi aliyewahi kuwa Naibu Waziri na mbunge Mstaafu wa Jimbo la Mpwapwa Mkoani Dodoma Bw. Gregory Teu kufuatia vifo vya watu hao 13 ambao ni ndugu wa familia yake waliopoteza maisha katika ajali ya gari iliyotokea nchini Uganda.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.