Waratibu wa wilaya za mikoa ya Njombe, Mbeya na Iringa wametakiwa
kuifikishia jamii mafunzo waliyopokea kwa takribani siku tatu juu ya
kupambana na ugonjwa wa ulemavu wa ghafla unaosababishwa na kirusi
hatari anaefahamika kwa jina la KIRUSIPOLI.
Agizo
hilo limetolewa na Afisa mfuatiliaji wa magonjwa yanayozuilika kwa
chanjo Honest Nyaki wakati akihitimisha mafunzo hayo yaliyotolewa kwa
siku tatu mkoani njombe kwa waratibu wa wilaya ambayo yanalenga
kuielimisha jamii jinsi ya kuepukana na magonjwa yanayozuilika kwa
chanjo.
Zoezi la utoaji mafunzo linafanyika
nchi nzima kwa lengo la kutokomeza na kuelimisha jamii hasa katika kuwa
na ufahamu juu ya magonjwa ya ulemavu wa ghafla ambao dalili yake kuu ni
mwili kulegea na kuwa tepetepe dalili ambayo inatambulisha ugonjwa huo
wa ulemavu wa ghafla ambao unasababishwa na kirusi kinachofahamika kama
KIRUSIPOLI ( POLIO VIRUS ) kinachopatikana na kwenye kinyesi.
TAARIFA NA AMIRI KILAGALILA
POLIOVIRUS
ndio jina halisi la kirusi hicho ambacho kwa lugha ya kiswahili
kinafahamika kama KIRUSIPOLI , Kwa mujibu wa mtaalamu ambae ni afisa
ufuatiliaji wa magonjwa yanayozuilika kwa chanjo anasema kuwa kirusi
huyu ni hatari na amekuwa akiwakumba hasa watoto walio na umri chini ya
miaka kumi na mitano .
CUE....................................................MTAALAMU.
Aidha
jamii imetakiwa kuchukua hatua za haraka pindi wanapoona mtoto
anadalili hiyo kuu mwili kulegea na kuwa tepetepe basi wachukue hatua za
kuripoti katika vituo vya afya ili hatua za vipimo ziweze kufuata
kwaajili ya matibabu ya mtoto.
CUE ......................................................WITO KWA JAMII.
Mwaka
1996 nchini tanzania mgonjwa wa ulemavu wa ghafla alipatikana kwa mara
ya mwisho ambapo mpaka sasa hakujatokea tena mgonjwa au mwathirika wa
ugonjwa huo hali ambayo imewalazimu watalaamu kuchukua hatua za kufanya
uchunguzi kwaajili ya kutafuta kama ugonjwa huu upo ili kuweza
kuuteketeza kabisa kwaajili ya usalama wa afya za watoto.
CUE............................................................UKUBWA WA TAITIZO LA ULEMAVU WA GHAFLA
Pius
Willium Yonga na Dr.Huruma ni miongoni mwa waratibu ambao wamehudhuria
katika mafunzo hayo ya siku tatu hapa mkoani njombe , ambao wanasema
kuwa wameyapokea mafunzo kwa mikono miwili huku wakiahidi kuyapeleka
mafunzohayo kwa jamii na kueleza kuwa mafunzo hayo ni muhimu kutokana na
mpango uliopo wa kutokomeza magonjwa ya ulemavu wa ghafla pamoja na
surua nchini tanzania.
CUE............................................................WARATIBU.
Hata
hivyo jamii imetakiwa kuwa na matumizi sahihi ya vyoo bora ili
kuhakikisha kuwa kirusi cha ugonjwa wa ulemavu wa ghafla hakipewi nafasi
katika kuwadhuru watoto.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.