ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, September 20, 2017

MKUU WA WILAYA YA KIBAHA ALAANI VIKALI VIONGOZI KUPIGWA RISASI,UTEKAJI WA WATOTO NA KUMTOLEA RAIS MANENO MACHAFU

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake kuhusina na kulaani  matukio ya vitendo vya kushambuliwa  kwa viongozi kwa risasi, utakeji wa watoto sambamba na kukemea tabia ya baadhi ya watu wanaotoa maneno machafu kwa Rais Dk Joh Pombe Magufuli.
(PICHA NA VICTOR MASANGU) 

NA VICTOR MASANGU,  
GSENGO BLOG
 KIBAHA PWANI

MKUU wa   Wilaya ya Kibaha  Assumpter Mshama amelaani vikali vitendo vya matukio ya baadhi ya watu kuwavamia na kuwashambulia kwa risasi viongozi na pia hakusita kukemea tabia ya utekaji wa watoto pamoja na wale ambao wamekuwa wakimtolea maneno machafu Rais wa awamu ya Tano Dk John Pombe Magufuli kitu ambacho kinamuumiza na anachukizwa nacho.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na matukio yanayoendelea katika sehemu mbali mbali Mkuu huyo alisema kwamba anasikitishwa kuona vitendo kama hivyo vinaendelea kufanyika katika jamii ya watanzania hali ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kwa wananchi kuishi  wakiwa katika hali ya hofu.

Mkuu huyo alisema kuwa baadhi ya watu kwa sasa  wamekuwa wakiamua kumtolea maneno machafu kiongozi wan chi bila ya kufahamu kuwa ni kinyume kabisa na sheria na taratibu za nchi kwa hivyo tabia kama hiyo haifai hata kidogo katika jamii na badala yake watanzania wanatakiwa kuwa wazalendo na nchi yao.

“Hivi karibuni ndugi waandishi mimi nachukizwa sana na kuona matukio mbali mbali yaiendelea hapa nchini, kama vile watoto kutekwa nyara, baadhi ya viongozi kupigwa risasi kwa kweli hii sio sahii kabisa hta kidogo na wengine kutoa maneno machafu kwa kiongoiz wetu wa  nchi kwa hili mimi nina laani vikali kabisa .

“Na kitu kingine napenda kuchukua fursa hii kumpa pole Mwanasheria wa Chadema Tundu Lissu kwa kuvamiwa na kushambuliwa na risasi za moto  na kumjeruhi vibaya na watu wasiojulikan, huyu Tundu Lissu ni kiongozi mkubwa na ni mtu maarufu zana hapa kwentu Tanzania lakini kitendo cha kushambuliwa na risasi sio sahii hata kidogo na mimi namwombe kwa Mungu apone na arudi kuendelea na Majukumu yake ya kuwatumbikia wananchi wa jimbo lake,”alisema.

Pia  katika hatua nyingine amebainisha kuwa serikali Wilayani Kibaha Mkoani Pwani inatarajia  kuvifutia rasmi hati viwanja zaidi ya 754 ambavyo  baadhi ya watu wamevitelekeza na kushindwa kabisa kuviendeeza kwa kipindi  cha muda mrefu hali ambayo imepelekea  kwa sasa maeneo  mengine   yamegeuka kuwa ni vichaka na  mapori makubwa ambayo yamekuwa ni kimbilio la kujifichia wahalifu pindi wanapofanya matukio ya wizi.

Tamko hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha   Assumpter Mshama wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake  kuhusiana na changamoto mbali mbali zilizopo katika suala la umiliki wa maeneo pamoja na mikakati waliyojiwekea katika kuhakikikisha maeneo ambayo hayaendelezwi yanarudishwa katika mikono ya serikali.

Mkuu huyo wa Wilaya alibainisha kwamba katika kuhakikisha anakabiliana na tatizo hilo tayari  ameshamwandikia barua Waziri wa ardhi William Lukuvi  kwa lengo la kuweza kumjulisha orodha ya watu ambao wameshindwa kabisa kuviendeleza viwanja hivyo hadi kufikia hatua ya kuwa mapori makubwa.

Nao baadhi ya wananchi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani akiwemo Elfasi Msuya na Zakharia Cheze wakizungumza na mwandishi wa habari hizo kuhusina na tamko la Mkuu wa Wilaya kufuta umiliki wa viwanja visivyoendelezwa wamepongeza hatua hiyo ya serikali  kwani itaweza kuwapa fursa wananchi wa hali ya chini waweze kujenga makazi ya kuishi.

WILAYA ya Kibaha mkoani Pwani kwa sasa bado inakabiliwa  na changamoto ya kuwa na idadi kubwa ya viwanja ambavyo vimetelekezwa na kutoendelezwa kwa zaidi ya miaka  15 hivyo kusababisha kuwepo kwa  vichaka na mapori  makubwa ambayo yanahatarisha usalama wa wananchi kutokana na wahalifu kujificha katika maeneo hayo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.