ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 12, 2017

SEKTA YA UREMBO JIJINI MWANZA YAPATA MWEKEZAJI WA NGUVU NI ROSLY BEAUTY STUDIO.

MGENI rasmi Mbunge wa jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula akikata utepe kuashiria uzinduzi wa studio mpya ya kisasa kwaajili ya kunakshi katika masuala ya urembo kwa viwango vya juu kwa akinamama na akinadada katika hafla iliyofanyika hivi karibuni jijini Mwanza, pembeni ni mkurugenzi wa Rosly Beauty Studio Bi. Alphoncina. Salon hiyo ya kisasa inapatikana barabara ya Hesawa, Jengo la Afya Radio, pande za Capri Point Nyamagana jijini humo. 

Katika hotuba ya ufunguzi aliyoitoa Mhe. Mabula amesema taifa linapo sisitiza wananchi wake kuchangamkia fursa hivi ndivyo inavyo maanishwa, ajira moja kubwa inaweza kuzalisha ajira kwa vijana wengine ..... "Ili kupata mafanikio vijana hatuna budi kushikana mikono na sote tukatembea pamoja, Alphoncina lazima tumsapoti, tusipomsapoti hatoendelea, biashara itasimama na ikisimama, hatutokuwa na kitu cha kujivunia" ZAIDI BOFYA PLAY KUMSIKILIZA ALICHOSEMA
Mkurugenzi wa Rosly Beauty Studio Bi. Alphoncina amesema kuwa moja ya sababu za uwekezaji wake ni kutaka kuupaisha mkoa wa Mwanza kwenye level zinazo hitajika kitaifa na kimataifa, saloon nyingi zimekuwa za viwango vya chini nazo huduma zikitolewa bila weredi wa fani, ameona uhitaji wa wakazi wa Kanda ya Ziwa ni makubwa hivyo akaamua kuja na kitu kipya chenye viwango na unafuu katika bei.
Kabla ya uzinduzi wa Rosly Beauty Studio, Saloon ya kisasa inapatikana eneo la Capri Point Nyamagana jijini Mwanza.
Kabla ya uzinduzi wa Rosly Beauty Studio, Saloon ya kisasa inayopatikana eneo la Capri Point Nyamagana jijini Mwanza.
Msimamizi katika ujenzi Kabula Kazi alifunguka juu ya changamoto za mafundi wakati wa ujenzi wa Rosly Beauty Studio, Saloon ya kisasa iyonapatikana eneo la Capri Point Nyamagana jijini Mwanza.
Rose Lulangwa ni mmoja wa wanawake wawekezaji katika sekta ya upambaji jijini Mwanza akitoa uzoefu wake jinsi alivyo pambana kwenye ujasiliamali hata hii leo akiwa ni shuhuda wa kazinzuri ya mdogo wake katika kazi mwekezaji mpya wa Rosly Beauty Studio, Saloon ya kisasa iyonapatikana eneo la Capri Point Nyamagana jijini Mwanza.
Pale sisters wanapokutana what do you expect....?
 Mwanabure ambaye ni sasa ni mwekezaji mkubwa wa sekta ya uokaji vitafunwa jijini Mwanza akifunguka juu ya uzoefu wake.
Sisters ndani ya hafla.
Mvinyo nao ulihusishwa kunakshi furaha za wadau waliohudhuria uzinduzi wa Rosly Beauty Studio.
The area.
Flowers.
Mgeni rasmi Mbunge wa jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula akisaini kitabu cha uzinduzi mara baada ya kukamilisha zoezi hilo eneo la Capri Point Nyamagana jijini humo.
Muonekano wa ndani wa Rosly Beauty Studio. Salon ya kisasa inayopatikana Capri Point Nyamagana jijini Mwanza.
"Karibu tukuhudumie"
"Wewe ni mtu muhimu sana kwetu"
Huduma nadhifu ziko hapa iwe kwa maharusi, wadau kawaida au kwa mitoko ya usiku basi hakuna tena shida.
Mambo ya massage.
Bango linasema na wewe.
Hafla ilipendeza nao waalikwa wali-enjoy vya kutosha.

Tufuate kupitia instagram @makeupbyrosly_mwanza

About Rosly Beauty Studio


The Beauty Studio is set inside Afya Radio department in Capri Point Nyamagana Mwanza.

Bi. Alphoncina established the business 4th of this August 2017 and her highly skilled team. They pride themselves on their strong local reputation for luxury professional treatments in a friendly, relaxing setting. They only use the latest techniques and products.


The Rosly Beauty Studio team are dedicated to providing you with professional services to help you look and feel amazing whether it is a new set of acrylic nails or a relaxing massage.
KARIBU SANA.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.