ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 4, 2017

SAIDA KAROLI ALISIMAMISHA JIJI LA MWANZA KWA MUDA, KESHO KUFANYA YAKE CCM KIRUMBA.

 Mwanamuziki nguli wa muziki asili nchini Tanzania leo asubuhi amewasili jijini Mwanza na kupata mapokezi makubwa kutoka uwanja wa ndege jijini hapa. Mamia ya wananchi wa viunga mbalimbali wakifuatilia matangazo ya moja kwa moja kutoka eneo la tukio kuitia Jembe Fm waliitikia kujitokeza kwenye njia mbalimbali na kumlaki mkali huyo.
Saida Karoli katika ardhi ya jiji la Mwanza kwaajili ya show yake itakayofanyika jumamosi hii ya tarehe 5 August 2017 katika uwanja wa CCM Kirumba.
Saida Karoli nje ya uwanja wa ndege Mwanza.
Mkurugenzi wa Jembe Media Group Dr. Sebastian Ndege kushoto akihakiki wasanii na wanamuziki waliowasili viwanjani hapo. Katikati ni mwanahip hop kutoka kundi la WEUSI G.Nacko akishow love na mratibu Hellen Kazimoto.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Jembe Media Group Dr. Sebastian Ndege, G. Nacko na Hellen Kazimoto.
Mambo ni motto.
The Crew.
Msafara wa mapokezi wa wasanii waliotinga jijini Mwanza.
Mdau aka shabiki akikimbilia kushikana mkono na mwanamuziki Saida Karoli.
Hatua kwa hatua toka uwanja wa ndege wa Mwanza.
Viunga vya Ilemela na marafiki asubuhi na mapema leo hii.
Msafara.
Mbele marafiki wa usafiri wa bodaboda.
Jembe ni Jembe
Saida na mashabiki zake.
Mama mama ......hawa ni wachuuzi wa Samaki wanaofuatilia kazi za mwanamama Saida Karoli na ujio huu umekuwa kama faraja kwao.
Msafara wa Saida Karoli view toka juu ya daraja la Magufuli Mwanza.
Jembe Live.
Sisi.
Mapema asubuhi barabara ya Nyerere jijini Mwanza.
Katikati ya viunga vya jiji hapa ni Dampo.
Soko la Kirumba jijini Mwanza.
Mahaba ya wana wa nyumbani.
Nimerudi......
Aksanteni tukutane CCM Kirumba Mwanza kama ni viingilio tizama hapo chini.
Salaaam salaam katikati ya jiji la Mwanza.
Watoto nao wanamjua.
Hapa ilimlazimu kuzungumza japo kiduchu na wadau wake.

Na tuliamshEeee sasa ndani ya uwanja wa #CCMkirumba Jumamosi hii tarehe 5 August 2017 miaka 15 ya Salida Karoli. Kulia atasimama @chegechigunda kushoto @gnakowarawara juu @officialnandy na pale kati ni #WEWE shabiki usiyekosa show kali kama hizi.
Tsh 3,000/= WATOTO
Tsh 5,000/= KAWAIDA
Tsh 20,000/= VIP
 ▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬
Kama unamfahamu vyema na unaweza kumwelezea vyema #Saida_Karoli Muda wako sasa kuyaoga #MAKOMPLIMENTARI Mpango mzima powered by @jembenijembe sponsored by @Jembefm #Uhuru_Hospital #New_mwanza_Hotel #JambO #AirTanzania na @cloudsfm ▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.