ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 26, 2017

POLISI YAFANYA UCHUNGUZI MLIPUKO OFISI ZA WANASHERIA.

Muonekano wa mbele wa ofisi hizo huku moto ukiendelea kuwaka muda ulipita.

Ofisi za IMMMA Advocates zinazomilikiwa na  wanasheria Fatuma Karume na Lawrence Masha zilizopo Upanga jijini Dar es Salaam, zimewaka moto leo asubuhi huku chanzo kikiwa bado hakijafahamika. Chanzo cha moto huo na hasara iliyosababishwa, bado havijafahamika na habari zaidi zitaendelea kukujia.
Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya 

Dar es Salaam. Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya amethibitisha kushambuliwa ofisi za wanasheria za IMMMA saa 8 usiku wa kuamkia leo Jumamosi, Agosti 26.

Mkondya amesema polisi wanafanya uchunguzi kujua ni nini kilihusika katika tukio hilo la mlipuko.


“Tupo hapa eneo la tukio, uchunguzi unaendelea na ukikamilika tutawapa taarifa zaidi, ila hatujajua kama bomu limehusika,” amesema Mkondya.


Ameeleza hadi sasa hakuna watu wanaoshikiliwa kuhusika na tukio hilo.

Mmoja wa viongozi wa Kampuni ya IMMMA, Sadock Magai amesema hakuna wizi ambao umefanyika katika mali zilizokuwa ndani.


“Tuwaachie Jeshi la Polisi wafanye kazi yao,” amesema Magai.

 

Ofisi za wanasheria wa kampuni hiyo zipo Barabara ya Umoja wa Mataifa eneo la Upanga jijini hapa.


Miongoni mwa wamiliki wa kampuni hiyo ni Fatma Karume, ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume. 


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.