ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, August 1, 2017

NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI ZASHAURIWA KUTUNGA SHERIA MPYA KULINDA ZIWA VICTORIA

NA ZEPHANIA MANDIA.


Nchi za jumuiya ya afrika mashariki zimeshauriwa kutunga sheria moja itakayosimamia utunzaji wa mazingira ya bonde la ziwa Victoria ili kuimarisha uhifadhi wa bonde la ziwa hilo ambalo linategemewa kiuchumi na kijamii  na zaidi ya watu millioni 44.


Akizungumza na waandishi wa habari, katibu mtendaji wa kamisheni ya bonde la ziwa Victoria DK.ALLI SAID MATANO amesema kuwa uwepo wa sheria moja utasaidia kutatua changamoto zinazolikabili bonde hilo ikiwemo ongezeko la shughuli za kibinadamu tofauti na sasa ambapo kila nchi inasheria yake.  


Ziwa Victoria ambalo ni kubwa kuliko yote barani afrika katika miaka ya hivi karibuni limekuwa likikabiliwa na tatizo la uharibifu wa mazingira na hivyo kutishia uendelevu wa ziwa hilo.


Katibu mtendaji wa kamisheni ya bonde la ziwa Victoria DKT.ALLI SAID MATANO amesema kuwa tishio la uendelevu wa ziwa Victoria limechangiwa na ukosefu wa sheria moja ya uhifadhi wa mazingira ya ziwa hilo miongoni mwa nchi wanachama.


Kufuatia hali hiyo DK.MATANO amelishauri bunge la jumuiya ya afrika mashariki kuharakisha mchakato wa kutunga sheria ya utunzaji wa mazingira ya bonde la ziwa Victoria ili kuwezesha nchi za jumuiya hiyo kuwa na sheria moja itakayosimamia utunzaji wa mazingira ya bonde la ziwa hilo.


Licha ya changamoto hiyo lakini mratibu wa mradi wa utunzaji wa mazingira katika kamisheni ya bonde la ziwa Victoria DK.DOREEN OTHERO amesema kuwa mafanikio yaliyopatikana hadi sasa si haba.


Bonde la ziwa Victoria lina ukubwa wa zaidi ya  kilometa za mraba laki moja zinazopatikana katika nchi za Tanzania,Uganda,Kenya,Rwanda na Burundi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.