ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 3, 2017

MGODI WA ACACIA BULYANHULU WALIPA ( 226,928,115,76 )KAMA USHURU WA HUDUMA KWA HALMASHAURI YA NYANG'HWALE

Meneja Mkuu wa Mgodi wa ACACIA Bulyanhulu  Graham Crew  Akikabidhi hundi  ya Fedha kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale  . Hamim Gwiyama pamoja na viongozi wa Halmashauri hiyo akiwemo Mbunge wa Jimbo hilo ,Hussein Amar Kasu

Meneja Mkuu wa Mgodi wa ACACIA Bulyanhulu  Graham Crew,akizungumza juu ya wao kama mgodi kuendelea kushiriki kwenye swala la maendeleo kwenye Wilaya hiyo.

Wilaya ya Nyang'hwale  . Hamim Gwiyama,akielezea juu ya hatua hiyo na pia amewashukuru kwa kuendelea kuwa wahaminifu kwa kulipia kodi ambayo itasaidia kufanya shughuli za  maendeleo Wilayani Humo.

Baadhi ya wadau wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyo wakati alipokuwa akizungumza.

NA JOEL MADUKA WA MADUKA ONLINE


Mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu ambao upo kwenye Halmashauri ya Msalala Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga ,umekabidhi hundi ya yenye thamani ya shilingi milioni mia mbili na ishirini na sita,laki Tisa ishirini na nane Elfu na mia moja kumi na tano na senti sabini na sita(226,928,115,76) kwa ajili ya ushuru wa huduma kwa halmashauri ya Nyang’hwale.

Kiasi hicho cha fedha ni asilimia 33% ya malipo ya ushuru wa huduma kwa ajili ya kipinidi cha miezi sita yaani Januari hadi mwezi Juni mwaka Huu ,kiasi ambacho ni asilimia 0.3 ya ukokotoaji wa ushuru wa huduma kwa mgodi huo kwa kipindi husika.

Akikabidhi hundi  hiyo,Meneja Mkuu wa Mgodi Huo ,Graham
Crew,amesema kuwa jumla ya malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha miezi sita iliyopita ni shilingi za Kitanzania ,Milioni mia sita ,themanini na saba,laki sita na sitini elfu ,mia tisa hamsini na sita na senti themanini na nne (687,660,956,84) na kwamba malipo hayo yamegawanywa kwenye halmashauri mbili  Kwa Mujibu wa makubaliano na serikali ambapo Halmashauri ya Msalala imepata asilimia 67%  na  Nyang’hwale  33% hivyo katika kiasi hicho ,halmashauri ya Msalala imelipwa kiasi cha Shilingi Milioni mia nne  sitini,laki saba thelathini na mbili Elfu mia nane arobaini na moja na sent inane(460,732,841.08) .

Aidha kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,Carlos  Gwamagobe,amesema kuwa fedha ambazo zimekuwa zikitolewa zinasaidia katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kujenga madarasa na kukarabati majengo ambayo ni chakavu.

Mkuu wa Wilaya Hiyo,Hamim Gwiyamba ,amekili kuwepo kwa athari kutokana na mapato kupungua kwa kiasi kikubwa kutoka kwenye mgodi wa acacia na kwamba kuna huduma za maendeleo zinaweza kupunguzwa kutokana na kupungua kwa Fedha.

Hadi sasa mgodi huo umelipa zaidi ya Shilingi Bilioni 10,200,000,000 tangu mwaka 2000 kama kodi ya ushuru wa huduma.Kampuni ya Acacia ilianza kutoa malipo ya ushuru wa huduma wa asilimia 0.3 ya mapato ghafi kwa halmashauri  husika mwaka 2014,kutoka kiasi cha Dola 200,000 kwa mwaka iliyokuwa inalipwa kama kodi ya ushuru wa huduma ya miaka ya nyuma.

IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.