ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 10, 2017

KILIMO CHA MKATABA KUONGEZA UZALISHAJI ZAO LA PAMBA

Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba Tanzania TCB James Shimbe akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya Nane nane Nyamongholo wilayani Ilemela mkoani Mwanza.

Wakulima wa pamba nchini wamehimizwa kujiunga na kilimo cha mkataba kwa kuwa kina faida na mafanikio kwa wakulima na Taifa kwa ujumla.

Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba Tanzania TCB James Shimbe amesema kilimo cha Mkataba kimesaidia kuongeza wigo wa eneo la uzalishaji wa pamba na matumizi ya mbegu bora ya UKM 08.

Pia amesema kilimo hicho kimesaidia kusukuma usambazaji wa matumizi ya pembejeo muhimu za zao hilo ikiwemo viwatilifu na upatikanaji wa huduma za ugani.
Mbegu aina ya UKM 08.
Kilimo cha Mkataba kimewafanya wakulima wa ukanda wa Magharibi wanaojumuisha mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Geita, Mara Tabora, Singida, Kagera na Kigoma kupata usimamizi mzuri wa sheria na sera za kilimo kupitia maofisa ugani walioko kwenye halmashauri zao za wilaya.

Kilimo hicho pia kimesaidia kuongeza eneo la uzalishaji wa zao la pamba, matumizi makubwa ya mbegu za kupanda ingawa bado juhudi zaidi zinahitajika ilikuhakikisha wakulima wengi zaidi wanajiunga na kuzingatia kanuni za kilimo bora cha pamba.
Moja kati ya changamoto ambayo bodi ya pamba imeendelea kukabiliana nayo ni namna ya kuwafikishia elimu ya kilimo bora wakulima na elimu ya kilimo cha Mkataba, ambapo kumekuwepo na ushindani wa wanasiasa na wafanyabiashara ambao wamekuwa wakijinufaisha kupitia migongo ya wananchi kwa upotoshaji na kupinga hatua ya kilimo cha Mkataba.
Tayari elimu inaendelea kutolewa ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha wakulima namna ya kulima kwa kuzingatia vipimo na maelekezo yanayopendekezwa na wataalamu wa kilimo.
Maonesho yakiendelea taswira na ufafanuzi.
Uzalishaji wa mbegu kupitia madaraja.
"Tunawasisitiza sana kuacha kuchanganya pamba na mahindi katika upandaji ndani ya shamba moja na pia wasiweke maji na mchanga kwenye pamba ili kuongeza uzito kwani hicho ni kikwazo kingine kinachosababisha kushusha thamani ya pamba yetu kwenye soko la dunia" alisema James Shimbe.

"Lakini pia tunawahimiza wang'oe na kuchoma moto miche ya pamba baada ya kuvuna kwa kuwa wakiiacha inakuwa mazalia ya wadudu waharibifu wa pamba"
Madaraja ya pamba katika maonesho ya Nane nane Mwanza.
Maeneo ynayolima pamba.
"Katika kilimo hiki wakulima wanapaswa kutambua kuwa tija kilimo ikiongezeka mara dufu, kipato cha wananchi pia kitaongezeka. Hivyo basi lazima iwepo mikakati ya pamoja ya kuongeza uzalishaji kwa kushirikiana na wakulima, wachambuaji wa pamba, viongozi wa ngazi ya wilaya na Serikali kuu" Alisema Shimbe.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.