ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 9, 2017

KERO YA MAJI IBISABAGENI SENGEREMA



WAKAZI WA KITONGIJI CHA BUKALA KATA YA IBISABAGENI WILAYANI SENGEREMA WAMEIOMBA SERIKALI KUWATATULIA KERO YA MAJI  KATIKA KATA HIYO INAYOENDELEA WAKATI MRADI MKUBWA WA MAJI UMESHAZINDULIWA WILAYANI HUMO 

Malalamiko hayo yametolewa na wakazi hao katika mkutano wa vitongoji vitano kwenye kata hiyo vilivyokaa kujadili jinsi ya kutatua kero mbalimbali katika eneo hilo likiwemo swala la maji na kuiomba serikali kutatua changamoto hiyo

Wakizungumzia adha wanayoipata kutokana na kero hiyo bi Pendo Doto na bi Mary Karoli wao wamesema inawalazimu kuamka saa tisa usiku kwenda kisimani, na kutanguliza ndoo zao na madumu hali ni mazingira hatarishi na siyo kuvamiwa tu bali pia baadhi yao wamewahi kuumwa na nyoka hali ambayo inawafanya kuishi maisha ya hofu.

Kwa upande wake balozi Faida Yusuph amesema mwenyekiti wa serikali ya mtaa amekuwa akiwalaghai kwa kuahidi kutatua kero hiyo na hadi sasa hakuna kilichofanyika

Nayebalozi Joseph  Agustine amekiri kuwepo kwa kero hiyo na kuongeza kuwa kumekupo gari la serikali linalopitisha maji na kuyapeleka kwa watumishi waserikali wanaoishi maeneo hayo na kuwaacha wananchi wakiangaika

Aidha bwana Joseph amesema maji hayo ya kisima yanayotumika kwa sasa si safi na si salama na wananchi wako tayari kuchangia upatikanaji wa miundombinu ili kutatua kero hiyo

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.