ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 2, 2017

BAYERN MUNICH Vs LIVERPOOL 0-3 ALL GOALS & Highlights - Friendly 01/08/2017 HD

Bayern Munich vs Liverpool 0-3 - All Goals & Highlights - Friendly 01/08/2017 HD 

KOCHA wa Liverpool Jurgen Klopp baada ya kufanya vyema katika mechi za kujipima nguvu ikiwepo ya jana kuibandua Bayern Munich kwa rungu 3 bila majibu, anasema kuwa kikosi chake kinaweza kushinda ligi baada ya bahati mbaya ya msimu uliopita.

Liverpool ilianza msimu wa 2016-17 vizuri na walikuwa pointi sita pekee nyuma ya viongozi na hatimaye bingwa wa ligi Chelsea mnamo mwezi Januari.

Lakini walirudi nyuma baada ya kupata ushindi mmoja mwezi Januari na Februari kabla ya kumaliza katika nafasi ya nne pointi 17 nyuma ya Chelsea.

''Tutashiriki mechi za ubingwa.hatutaki kuanza msimu bila kuwa na lengo lolote'', alisema Klopp.
"Lazima tuwe na lengo na nadhani tuna timu nzuri sana sasa.tulikuwa na bahati mbaya msimu uliopita''.

''Nadhani tunaweza kucheza vyema .Tuwe na matumaini kwamba kila kitu kitakuwa shwari. Klop alisema kuwa kwamba mchezaji Phillipe Coutinho hauzwi, licha ya Barcelona kumtaka''.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.