ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 13, 2017

WALIOISABABISHIA SERIKALI HASARA YA BIL 12.7 WAACHIWA HURU.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru Kamshna wa zamani wa Mamalaka ya Mapato Tanzania (TRA),  Tiagi Masamaki na wenzake watano.

watuhumiwa hao walikuwa washtakiwa kwa tuhuma za uhujumu uchumi ambapo waliidaiwa kuisababishia Hasara Serikali  Shilingi Bilion 12.7.


Mbali na Masamaki washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo  iliyotokana na sakata la makontena 329 ni Meneja Kitengo cha Huduma za Ushuru  TRA, Habib Mponezya  (45) na Meneja Msimamizi na Ufuatiliaji wa Forodha, Burton  Mponezya (51).

Msimamizi Mkuu Kitengo cha Ushuru wa Forodha  ICD Azam, Eliachi  Mrema (31),  Mchambuzi  Mwandamizi  wa Masuala ya Biashara  TRA,  Hamis Omary (48), Meneja wa Oparesheni  za Usalama na Ulinzi  ICD, Raymond Adolf Louis (39) na Meneja wa Azam ICD, Ashrafu Khan (59) na Haroun Mpande (28) wa kitengo cha Mawasiliano ya Kompyuta ICT TRA.

Kwa pamoja wanadaiwa kuwa kati ya Juni Mosi na Novemba 17, 2015 walikula njama kwa kuidanganya serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu Sh 12.7 bilioni.

Washtakiwa hao, wanadaiwa ku danganya kuwa Makontena 329 yaliyokuwepo katika Bandari Kavu ya Azam (AICD) yalitolewa baada ya kodi zote kufanyika wakati wakijua si kweli.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.