ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 17, 2017

VIONGOZI CHADEMA WAACHIWA HURU.

NYASA, RUVUMA: Katibu Mkuu wa Chadema, Vincent Mashinji, wabunge wawili wa chama hicho na viongozi wengine  sita wa chama hicho waliokamatwa juzi na Jeshi la Polisi wilayani Nyasa, mkoani Ruvuma leo wameachiwa huru.

Afisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene amethibitisha kuachiwa huru kwa viongozi hao akiwemo Katibu Mkuu ,  Vincent Mashinji, Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe na Mbunge wa Viti Maalumu, Zubeda  Sakuru kwa kile kilichoelezwa kuwa ni maagizo aliyopewa ODC wa Nyasa kuwakamata viongozi hao na kuwaweka selo kwa saa 48.

Wengine waliokuwa wamekamatwa ni;

1. Philbert Ngatunga (Katibu wa Kanda)

2. Ireneus Ngwatura (M/kiti Mkoa)

3. Delphin Gazia (Katibu Mkoa)

4.Asia Mohamed (Afisa Kanda)

5. Cuthbert Ngwata (M/kiti Wilaya)

6. Charles Makunguru (Mwenezi Wilaya)

Kwa mujibu wa taarifa ya awali, polisi walivamia kikao cha ndani cha Chadema kilichokuwa kikiendelea mjini hapo ikiwa ni sehemu ya ziara ya Dk. Mashinji ya kukagua shughuli za chama katika kanda hiyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.