ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 6, 2017

TANZIA:- MWANAMUZIKI SHAHBAN DEDE AMEFARIKI DUNIA

 MWANAMUZIKI mkongwe Shaaban Dede amefariki dunia leo saa mbili asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu kwa takriban wiki mbili, mwanae Hamad Dede amethibitisha.

Hamad Dede amesema mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Mbagala jijini Dar es salaam, na kwamba ratiba na taratibu zote zitatangazwa mara zitapokamilika kupangwa.

Marehemu Dede atakumbukwa kama mmoja wa wanamuziki nguli kutokea nchini Tanzania kwa sauti yake tamu na utunzi wa nyimbo mbalimbali zilizoshika chati akiwa na bendi mbalimbali zikiwemo Tabora Jazz, Bima Lee, Mlimani Park na Msondo Ngoma ambako alikuwa anatumikia hadi mauti yanamkuta.

 BLOG inatoa mkono wa rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na mashabiki wa Shaaban  Dede kwa kuondokewa na mkongwe huyu wa muziki.

Mola aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi - AMIN

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.